Tetesi zinasema mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anatazamia kumuona mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland katika klabu hiyo kwa muda mrefu.

Nyota huyo aliye na miaka 20- ana mkataba na klabu hiyo ya Bundesliga hadi mwaka 2024, lakini anaweza kuondoka kwa euro milioni 75 (£67m) mwaka 2022 kwasababu ana kifungu kinachomruhusu kufanya hivyo katika mkataba wake wa sasa.

Klabu za Ligi ya Primia zimeombwa kupunguza idadi ya mashabiki wanaoruhusiwa uwanjani hadi 1,000. Mamlaka ya usalama wa viwanja vya michezo imesema agizo hilo linastahili kuzingatiwa kwa muda hadi pale mashabiki 2000 wataruhusiwa uwanjani.

Tetesi zinasema winga Muingereza Angel Gomes, 20, anasema aliondoka Manchester United kutafuta mwanzo mpya baada ya kukataa ofa yao na kujiunga na Lille.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema Mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa Anderlecht Mbelgiji Marco Kana, 18, Liverpool ndio klabu anayotamani kujiunga nayo atakapoamua kuhama.

Kipa wa Fulham Marcus Bettinelli, 28, ananyatiwa na klabu kadhaa za Ligi ya Primia. Kipa huyo ambaye kwa sasa yuko Middlesbrough kwa mkopo, alijumuishwa katika kikosi cha kitaifa cha England na Gareth Southgate mwaka 2018.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa Burnley na Jamhuri ya Czech Matej Vydra, 28, anataka kuondoka Turf Moor ili kupata nafasi ya kucheza soka ya kikosi cha kwanza.

Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, ameahidi kuongeza msaada wake wa chakula kwa shirikala la watoto na kutoa wito kwa wachezaji zaidi wa soka kumsaidia mshambuliaji wa England na United Marcus Rashford, 23, katika kampeni yake ya kuwakinga watoto dhidi ya njaa.

 

Nicolas Tagliafico

Beki wa kushoto na nyuma wa Argentina Nicolas Tagliafico, ambaye amehusishwa na Chelsea na Manchester City, amekubali kurefusha mkataba wake na Ajax ambayo inatarajiwa kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28- kusalia katika klabu hiyo hadi angalau mwisho wa msimu .

Tetesi zinasema mkurugenzi wa kiufundi wa AC Milan Paolo Maldini amekiri kuwa anamtaka winga wa Ufaransa Florian Thauvin, 27, ambaye mkataba wake Marseille unakamilika mwaka 2021.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa