Mpango wa Chelsea kurejesha mashabiki dimbani pale Stamford Bridge umekutana na upinzani kutoka kwa kundi la mashabiki ambao wanakosoa gharama za tiketi.

Mashabiki hao wametaja kuwa £75 kwa mechi dhidi ya Leeds ni utumiaji mbaya kabisa wa mapenzi ya mashabiki kwa timu yao.

Kutokana na kuendelezwa kwa mapambano dhidi ya Corona, Chelse wanatarajia kuanza kuruhusu mashabiki hadi 2000 mwezi ujao, kwa mujibu wa muongozo wa serikali.

Mashabiki wametoa tamko lao baada ya kupata taarifa juu ya mpango wa kurejesha mashabiki na gharama za tiketi kwa mechi ya tarehe 8 Disemba dhidi ya Leeds.

Msisitizo wa mashabiki wa Chelsea ni kuwa mapenzi yao kwa timu yanatumika vibaya. Msimamo wa walalamikaji hawa ni kuwa klabu imeamua kulipisha pesa kubwa zaidi ya klabu nyingine ya Premia kwa kipindi hiki kigumu cha hali mbaya ya uchumi.

 


 

 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

  1. Ninafikiri wamefanya hivyo kutokana na kuzuia watu wengi kuingia uwanjana kwa wingi kwa sababu ya kukwepa mbanano Wa watu kwenye uwanja kuepusha maambukiri ya corona kwa wingi uwanjani pia kwasababu mashabiki wamelalamika kuhusu hilo taarifa itafika na watasuluisha kwa hio

  2. Kutokana na ugonjwa wa corona kulikumba mataifa mengi hali ya kiuchumi imeyumba hvyo basi kunawafanya vilabu vingi vya mpira kutafuta njia moja au nyingine kutatua hii changamoto huku wakisahau hata raiya wa kawaida kwa sasa pesa awana Chelsea watafute njia ya kuwafurahisha mashabiki wao sio kwakatamiza

  3. Uchumi wa Vilabu umeyumba baada ya kupata ridhaa ya kuruhusu mashabiki njia pekee kwa vilabu kujikwamua ni kuongeza gharama ya tiketi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa