Reading walimaliza ukame baada ya mechi tano za Championship bila ushindi kwa kuifunga Bristol City  bao3-1 kwenye dimbani Madejski.

Haikuwa rahisi kuchagua nani angeshinda kwenye kipindi cha kwanza. Reading walisonga mbele baada ya dakika tisa za kipindi cha pili Ovie Ejaria kumzidi ujanja Bentley.

City walisawazisha kupitia Nahki Wells dakika ya 73 lakini Reading walipata bao la kuongoza wakati Meite alipowazawadia nyumbani dakika tatu baadaye.

Lucas Joao alikuwa mfunga dimba kwa kumaliza shughuli ya kufunga mabao dakika za mwisho, kwa kupitia krosi ya Meite na kumdungua Bentley.

Hatimae Reading Wamaliza Ukame wa Ushindi

Reading wameanza walianza vyema kampeni walipofungua kwa ushindi wa mechi saba, na mbio za mechi 7 za kutofungika zilifika tamati ghafla kwa vipigo vinne mfululizo kabla ya kumaliza sare ya 1-1 huko Millwall Jumatano usiku.

City pia ilikuwa imeanza vizuri msimu wa 2020-21, wakipata ushindi mara nne mfululizo, lakini kutoshinda kwenye mechi tano mfululizo uliwafanya kushuka hadi nafasi ya 10.


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

18 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa