Schalke wamemfuta kazi Manuel Baum kama kocha mkuu baada ya kutumkikia kibarua chake kwa siku 79 tu.
Huub Stevens, ambaye ni raia wa Uholanzi ndiye atakayechukua kibarua kwa mara ya nne, wakati klabu ikiwa chini ya msimmo wa Ligi ya Kuu ya Ujerumani -Bundesliga na wakiwa hawajashinda hata mechi moja katika michezo 28.
Huyu anakuwa bosi wa tatu wa Schalke msimu huu, Baum, ambaye alisimamia michezo 10, alichukua nafasi ya David Wagner mnamo Septemba.
Stevens, mwenye miaka 67, ni legendari wa klabu hii ya Ujerumani ambaye alifanikiwa kuwaongoza kutwaa ubingwa wa UEFA miaka ya 1996-97.

Mara ya mwisho alirejea Schalke wakati Domenico Tedesco alipotimuliwa Machi 2019 na kuiongoza timu kushinda 4-2 kwa wapinzani wao Borussia Dortmund, akiwasaidia kuepuka na kushuka daraja.
Meneja huyu anayechukua nafasi, alishaweka wazi kuwa hatokuja kurejea tena klabuni hapo. Lakini sasa amesema kuwa klabu yake inapomfuata katika kipindi kigumu anashindwa kukataa.
Schalke mara ya mwisho kuwa nje ya Bundesliga ni msimu wa 1990-91, na mpaka sasa wamebakiza michezo mitatu tu kuifikia rekodi ya ligi ya michezo 31 bila ushindi, ambayo iliwekwa na klabu ya Tasmania Berlin mnamo 1965-66.
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!



Hopemwaikuka
Kaz kweli kweli
Adelta
Hii ni Kali ya mwisho wa mwaka
warda
Schalke hawataki ujinga
Sarah
Duu hiyo kali
Dorophina
Kweli schalke wanataka maendeleo kwa haraka
Lydia Emmanuel Magoti
Duu wangempa mda kwanza wamekosea
Mwanahamisi
Duuh hiyo kali
Saupha mohamed
Dhuuu nomaa
Ester jackson
Kwa kweli wamefanya vizuri mana hiyo ndio sheria ukifanya vibaya lazima ufungashe virago
Tatu
Kali ya mwaka