Chan 2021: Tanzania Yaanza na Kipigo.

Mashindao ya kimataifa kwa wachezaji wa ndani – Chan 2021, yameanza kutimua vumbi nchini Cameroon. Tanzania imeanza kwa kipigo dhidi ya Zambia.

Taifa Stars wameshindwa kuitumia vizuri karata ya kwanza kwenye mashindano ya mwaka huu baada ya kuruhusu kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya wanachipolopolo.

Mchezo ulianza kwa timu zote kutokuwa na utulivu zikishindwa kutambua ni kipi hasa zinatafuta. Kipindi cha pili mambo yalibadilika, Stars walianza kutafuta nafasi za kufunga lakini Chipolopolo walizitafuta na kuzitumia vyema nafasi zao.

Shomari Kapombe aliushika mpira katika eneo hatari na kuwazawadia Zambia mkwaju wa penati kunako dakika ya 62. Sikombe aliitumia vyema nafasi hiyo na kuwapatia Zambia goli kupitia mkwaju wa penati.

Collins Sikombe (Zambia) akishangilia goli lake dhidi ya Tanzania.

Almanusura Sikombe apachike goli la pili katika dakika ya 75 lakini umahiri wa Aishi Manula uliwaokoa Stars baada ya kumzidi ufundi Sikombe ambaye alibaki yeye na kipa huyo.

Dakika ya 82, Zambia walimaliza mchezo baada ya Sikombe kutoa pasi maridadi kwa Chabula ambaye alipachika goli la 2 na kuwapatia Chipolopolo pointi 3 muhimu katika mchezo wa kwanza wa mashindano ya Chan 2021.

Stars sasa wanahitaji matokeo ya ushindi katika michezo miwili iliyosalia kwenye hatua ya makundi. Mchezo unaofuata, Stars watachuana na Namibia kabla ya kucheza na Guinea katika mchezo wa mwisho wa hatua za makundi.


USHINDI UPI NI MKUBWA KWAKO, £2,000,000? 🤑

Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.

INGIA MCHEZONI

20 Komentara

    Tusikate tamaa tujipange kwa mechi zinazokuja

    Jibu

    Zambia ni timu nzuri na inauzoefu wa mashindano haya. Ni imani yangu tutashinda dhidi ya Namibia na Guinea

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Tuongeze bidii tutashinda

    Jibu

    Tanzania inabidi ijipange vyema kwa ajili ya michezo ijayo

    Jibu

    Naamini bado wana nafasi yakufanya vizuri

    Jibu

    Tanzania wamekutana na timu nzuri ndiomaana ikapigwa

    Jibu

    Abali njema

    Jibu

    Kawaida ndio mchezo huo

    Jibu

    Pole yao

    Jibu

    Ndio mchezo ulivyo

    Jibu

    tuongeze bidii tutafanikiwa

    Jibu

    Sio mwisho wa mchezo wasikate tamaa

    Jibu

    Taifa stars jamani wamejuwa kutuumbua mashabiki wao.

    Jibu

    Ndo mchezo huwo

    Jibu

    Taifa 🌟 wanatakiwa wakaze

    Jibu

    Tanzania katika Soka ni kichwa cha Mwendawazimu

    Jibu

    Ndio mchezo ulivyo

    Jibu

    Watasonga tu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.