Roma wamejikuta wamefanya sabu nyingi zaidi ya idadi ya Sabu zinazotakiwa, ambazo ni sabu tano katika mechi ya Copa Italia dhidi ya Spezia
Sakata hili limetokea katika mechi ambayo walipoteza kwa bao 4-2 Jumanne, ushindi uliopatikana kwenye mda wa nyongeza.
Mechi ilikuwa ngumu na matokeo ya awali yalikuwa ni bao 2-2, kisha timu zikaingia kwenye mtanange wa mda wa nyongeza.

Sabu ambazo zinatakiwa kwa sasa, baada ya kupitiwa kwa muongozo mpya wa sabu na FIFA na pia shirikisho la soka Italia ni sabu 5 tu. Katika jitihada za kuutafuta ushindi Roma wakajikuta wamefikisha sabu 6, zaidi ya sabu zinazotakiwa.
Roma wamepoteza mechi hii kwa matokeo, lakini hata kama wangeshinda mechi hii, kwa mujibu wa taratibu wangekuwa wamepoteza nafasi moja kwa moja kwa kukiuka utaratibu wa sabu.
Roma wamekosa nafasi ya kuendelea na robo fainali, Spezia anaenda kukutana na Napoli kwenye robo fainali Januari 27.
Kocha Paulo Fonseca amekubali kuwa kulikuwa na kasoro katika mchakato wa kuamua nani aingie na kukamilisha zoezi hilo, hivyo ni suala ambalo wanatarajia kulizungumzia kwa kina zaidi ndani ya timu.
Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.



Adelta
Cha msingi Roma wasikate tamaa waendelee kujipanga ili kipindi kijacho wafike kwenye fainal
Sadick
Roma maji yalizidi unga wakajikuta wanaingiza wachezaji wengi kuliko wanaohitajika
Venerose
Asante kwa taarifa
Magdalena
Roma Wana kibarua kizito
Dorophina
Naona kama sabu zinawabana sana klabu
Lydia Emmanuel Magoti
Roma Wana kibalua kizito
Hopemwaikuka
Shughul mnayo
Sarah
Roma kazi wanayo
Angelina
Changamoto za mpira
felister
Roma shughuli wanayo
Neema juma
Mmh Roma ndomda wa kupambana upya
Sabrina
Duuh mtihani huo
warda
Wangewaacha tu makocha wamechanganyikiwa na Corona