Kocha wa Chelsea, Frank Lampard anaendelea kuwa matatani kutokana na matokeo mabovu ya kikosi chake.
Hii ni baada ya Chelsea kupoteza mchezo wa 5 kati ya 8 waliyocheza kwa siku za karibuni. The Blues walikuwa uwanjani jana usiku kupambana na Leicester City pale King Power Stadium.
Frank Lampard alishuhudia vijana wake wakiambulia kipigo cha magoli 2-0 dhidi ya vijana wa Brendan Rodgers. Kupoteza mchezo dhidi ya Leicester, kunaweka rehani kibarua cha kocha huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akilaumiwa kwa kushindwa kukiongoza kikosi hicho.

Frank Lampard alipatiwa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kufanya usajili na kuijenga upya Chelsea kwa ajili ya msimu huu. Mambo yanaendelea kuwa mabaya siku baada ya siku na sasa The Blues wanaporomoka mpaka nafasi ya 8 kwenye msimamo wa EPL.
Akizungumzia mustakabali wa kibarua chake ndani ya klabu hiyo, Lampard alisema “sina uwezo wa kuamua hilo. Nimekuwa nikiulizwa hili swali kwa wiki kadhaa sasa. Ninaelewa ni kwanini, ni matarajio ya klabu kama ni sawa au sio sawa.
“Niliichukua hii kazi nikijua kutakuwa na kipindi kigumu kutokana na kuwa na timu ambayo haipotayari kwa mashindano. Tulifungiwa (kusajili), tunawachezaji wadogo, tumesajili wachezaji wapya ambao tunaona wanajitahidi kuzoea mazingira.
“Tunachoweza kukifanya kwa sasa ni kuendelea kupambana.”
Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.



Sadick
Nadhani bado Abrahmovich ana imani nae lkn kama hali hii itaendelea mechi 2 au 3 zijazo atatupiwa virago
Adelta
Chelsea Bado wanakibarua kigumu
Venerose
Pole sana Frank
Magdalena
Lampard ana kazi kubwa ya kukipanga vyema kikosi chake
Dorophina
Lampard anazingua sana na kikosi chake
Lydia Emmanuel Magoti
Lampard sijui anakwama wapi
Hopemwaikuka
Had huruma
Sarah
Lampard Wana kazi kubwa
Angelina
Sijui itakuaje
felister
lampard kazi anayo
Neema juma
Jamani lampard!!!!!!.
Sabrina
Lampard tuliza mshono
Ernest Kimeru
Ilipofikia Lampard ndani ya hizi siku chache tutasikia jambo lake, Ameshindwa kuvaa Viatu ndani ya Chelsea mbali na usajili mkubwa uliofanywa na Chelsea, Sio kwa Mfumo wala Mbinu Lampard amegonga Mwamba
warda
Kawaida tu atakaa sawa