Blues wanaelekea Leicester katika Uwanja wa King Power Jumanne usiku wakiwa na hamu ya kuanza msimu wao baada ya kuanza kwa kuchechemea 2020-21.
Na bosi Frank Lampard atapewa nguvu kwa urejeo wa James aliyetoka kuuguza majeraha yake aliyoyapata Disemba 26.
Beki huyo wa kulia wa England, 21, hajacheza tangu tangu Chelsea ilipofungwa siku ya Boxing Day mikononi mwa Arsenal kwa sababu ya majeraha ya goti na misuli.
Lakini James sasa anatarajiwa kurudi kundini huko Midlands, akichukua nafasi ya Cesar Azpilicueta katika timu hiyo.
Andreas Christensen pia amerudi kutoka kwenye majeraha, lakini kuna uwezekano wa kufanya XI inayoanza.
Wasiwasi pekee wa majeraha ya Chelsea sasa ni kiungo nyota N’Golo Kante, ambaye hatarajiwi kuwa tayari kwa mchezo huo katika jiji la Leicester.
Lampard huenda akaanza na Edouard Mendy langoni, James na Ben Chilwell wakiwa katika nafasi za beki wa pembeni.
Antonio Rudiger anaweza kuimiliki nafasi ya ulinzi wa kati pamoja na Thiago Silva katika dimba la katikati la ulinzi.
Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.



Adelta
Pole Sana beki kwa majeraha
Sadick
Nafasi ya Reece James imezibwa vzr bado Chelsea haina beki imara ndio maana inafungwa sana
Venerose
Habari njema
Magdalena
Ngoja tuone kama lampard hatofanya makosa tena
Dorophina
James atakuja kwa Kasi sana baada ya kukosa michezo kadhaa
Rahmal
Habari njema
Lydia Emmanuel Magoti
James atakaa sawa tuu
Hopemwaikuka
Kila la heri
Sarah
Itakuwa vizuri
Angelina
Kila la kheri
felister
pole yake
Neema juma
Itakuwa vizuri sana
Ester mmakasa
Anatutia moyo sana mashabiki wake.
Sabrina
Duuh pole sana
warda
Ajikaze tu mana Leicester nao wako moto sana