Baada ya Robert Snodgrass kutemwa kwenye kikosi cha West Brom Albion dhidi ya West Ham United, Premier League kufanya uchunguzi kuhusu usajili wa mchezaji huyo.
Katika hali isiyo ya kawaida, Snodgrass hakujumuishwa kwenye kikosi cha West Brom kilichoambulia kipigo dhidi ya West Ham United jana usiku.
Kocha wa Albion, Sam Allardyce alizungumzia kilichotokea na kudai kuwa “ni makubaliano yaliyokuwa yamewekwa kati ya timu hizo wakati wa usajili wa Snodgrass”.
Taarifa rasmi ya usajili wa Snodgrass ilieleza kuwa mchezaji huyo alisajiliwa kwa mkataba wa moja kwa moja na sio mchezaji wa mkopo akitokea West Ham United.
Kwa mujibu wa sheria za usajili za Premier League, mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo – hawezi kucheza pale timu iliyomsajili itakapokutana na timu yake ya awali.
Japokuwa, kama mchezaji alisajiliwa kwa mkataba wa moja kwa moja – anaruhusiwa kucheza dhidi ya klabu iliyomuuza.
Kutokana na mkanjiko uliotokea kwa Snodgrass, Premier League (EPL) wanafanyia uchunguzi usajili wa mchezaji huyo licha ya kwamba EPL imesema wameridhishwa na taratibu za usajili zilizofuatwa baina ya vilabu hivyo.

Hii iliwahi kutokea kwa Tim Howard ambapo alisajiliwa Everton kwa mkataba wa moja kwa moja akitokea Man United, Februari 2007. Lakini Howard hakujumuishwa kwenye kikosi cha Everton kilichocheza na United April 2007 kutokana na makubaliano ya vilabu hivyo wakati wa usajili wa kipa huyo.
Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.



Magdalena
Duh hii ni balaa sasa
Angelina
Nice update
Rahmal
Abali njema
Adelta
Habari njema
Lydia Emmanuel Magoti
Habari nzuri
Dorophina
Mambo yashakuwa mengi
Hopemwaikuka
Mmh
Sarah
Habari nzuri
felister
mmmh
Neema juma
Habarii ziko poaa
Ester mmakasa
Ni makala ya kusisimua sana .
Janeflora malisa
Sawa t
Shakila mrope
Du ni hatari
Venerose
Mmmh kazi ipo
Sabrina
Duuh majanga
Ernest Kimeru
Kuna jambo nyuma ya pazia hapa
warda
Balaa tena