Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema Arsenal imeafikia makubaliano ya kumsani kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard, 22, kwa mkopo kutoka kwa Real Madrid. The Gunners wamekubali kulipa dau la £1.8m kumsajili Odegaard lakini hawatakuwa na fursa ya kifungu cha kumnunua katika kandarasi hiyo

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atamruhusu mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28, kuondoka kwa mkopo wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari lakini uamuzi wa mwisho utafanywa na bodi ya klabu hiyo ya Old Trafford.

Real Madrid huenda wakawa na hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund ,20, Erling Braut Haaland, ambaye anatakiwa na Chelsea na Man United baada mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kusema kwamba anafurahia kusalia Paris St-Germain.

 

Erling Haaland

Beki wa Manchester City’ na Uhispania Eric Garcia, 20, na kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30 wote wakiwa kandarasi zao zinakamilika mwisho wa msimu huu, wanalengwa na Barcelona licha ya mkufunzi wa klabu hiyo Ronald Koeman kukiri kwamba timu hiyo haipo katika nafasi ya kusajili wachezaji mwezi huu.

Tetesi zinasema Newcastle United inatarajiwa kuthibitisha uteuzi wa Graeme Jones kuwa kocha kumsaidia wa Steve Bruce, ambaye ameunga mkono usajili huo.

Tetesi zinasema hatma ya mshambuliaji wa Uturukji Cenk Tosun’ katika klabu ya Everton ipo mashakani baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kuwachwa nje ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Sheffield Wednesday katika kombe la FA siku ya jumapili.

Tetesi zinasema Billy Gilmour, 19, huenda akandoka Chelsea kwa mkopo mwezi huu licha ya kuanzishwa katika kombe la FA katika mechi ya ushindi dhidi ya Luton Town, kulingana na mkufunzi Frank Lampard.

Tetesi zinasema Mkurugenzi wa Real Madrid Emilio Butragueno ameonekana kuthibitisha kwamba kiungo wa kati wa Croatia mwenye umri wa miaka 35 Luka Modric atasaini kandarasi mpya katika klabu hiyo.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ameiomba bodi ya klabu hiyo kutokosa fursa ya kumsajili beki wa Austria na Bayern Munich, David Alaba, 28, wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu.

Liverpool inapigiwa upatu kumsaini mshambuliaji wa Derby County Kaide Gordon, 16, katika mkataba wenye thamani ya £1m, huku Man United na Tottenham zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa england.

Kiungo wa kati wa na Uholanzi Donny van de Beek, 23, yuko tayari kusalia katika klabu ya Old Trafford licha ya kupatiwa fursa chache kushiriki katika klabu hiyo licha ya kujiunga na miamba hiyo ya England kwa dau la £40m mwisho wa msimu huu.

Tetesi zinasema Klabu ya Fenerbahce imewataka mashabiki wake kusaidia kukusanya fedha kufuatia kusainiwa kwa mchezaji wa zamani wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, kutoka Arsenal.


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

14 Komentara

    Martin atawafaa sana Arsenal

    Jibu

    Mkufunzi wa Liverpool Yuko sahihi

    Jibu

    Tetesi zimekaa pouwa

    Jibu

    Tetesi ziko poa sana

    Jibu

    Tetesi zimebamba

    Jibu

    Arsenal nao waache maneno mengi maana kikosi chenyewe kishayumba

    Jibu

    Tetesi ziko poa

    Jibu

    Erling Braut Haaland anatakiwa kuchangamkia dili ya Real Madrid

    Jibu

    Arsenal wamefanya usajili mzuri sana

    Jibu

    Tetesi ziko poa

    Jibu

    Haalad njoo Man U

    Jibu

    Tetesi ziko poa

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Nice

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.