Mourinho : Kupishana kwa Wachezaji ni Jambo la Kawaida.


Jose Mourinho, Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham amesema kuwa kitendo cha wachezaji wake kukasirika ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo ni jambo la kawaida kutokea hasa pale ambapo timu inakuwa imefungwa.

Januari 28, Mourinho alikiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool na kukubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

Habari zimeeleza kuwa wakati wa mapumziko wachezaji walikuwa wakilaumiana huku zigo kubwa la lawama akipewa beki Serge Aurier kwa kuwa alishindwa kuongeza uimara kwenye safu ya ulinzi dakika za mwisho kabla ya mapumziko na kuruhusu Liverpool kupata bao la kuongoza.

 

Roberto Firmino alifunga bao hilo la kwanza kwa Liverpool akiwa chini ya uangalizi wa Aurier na Eric Dier ambao walikuwa kwenye safu ya ulinzi.

Mourinho aliamua kumfanyia mabadiliko Aurier ambaye alikasirika na anatajwa kuondoka uwanjani wakati wachezaji wenzanke wakiingia kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili na waliokota nyavuni mabao mengine mawili.

Pia inaelezwa kuwa nyota huyo inaweza kuwa ngumu kwake kubaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa amebakiza dili la miezi 18 kumaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo.

 

Jose Mourinho kuhusu kumtoa beki huyo amesema:-“Ulikuwa ni wakati mgumu na hali ambayo walikuwa nayo wachezaji na ilikuwa ni ngumu kuweza kukubali suala la kupoteza.

Ni ngumu kukubali hali hasa ya kufungwa mabao ila huwezi kuzuia namna ambavyo inatokea ndani ya uwanja hasa pale ambapo unapata nafasi ndani ya dakika moja. Ni kweli ni hali ya wachezaji hawakuwa na furaha hivyo ni jambo la kawaida,” .


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

13 Komentara

    Kawaida Sana…

    Jibu

    Ni kweli kabisa

    Jibu

    Kawaida

    Jibu

    Ni kweli kawaida na kama ikitokea hali kama hiyo inatakiwa uongozi uingilie Kati ili kuwaweka wachezaji sawa

    Jibu

    Kweli kabisa

    Jibu

    Ni kweli

    Jibu

    Mzee wakutoka tusha mzoea

    Jibu

    Duh uyu nae anatafuta sababu

    Jibu

    Kweli kabisa

    Jibu

    Mbona ndo maisha yetu hayo

    Jibu

    Akika ni kweli kabisa

    Jibu

    Kawaida

    Jibu

    kweli ni jambo la kawaida

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.