Jose Mourinho, Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham amesema kuwa kitendo cha wachezaji wake kukasirika ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo ni jambo la kawaida kutokea hasa pale ambapo timu inakuwa imefungwa.
Januari 28, Mourinho alikiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool na kukubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1.
Habari zimeeleza kuwa wakati wa mapumziko wachezaji walikuwa wakilaumiana huku zigo kubwa la lawama akipewa beki Serge Aurier kwa kuwa alishindwa kuongeza uimara kwenye safu ya ulinzi dakika za mwisho kabla ya mapumziko na kuruhusu Liverpool kupata bao la kuongoza.

Roberto Firmino alifunga bao hilo la kwanza kwa Liverpool akiwa chini ya uangalizi wa Aurier na Eric Dier ambao walikuwa kwenye safu ya ulinzi.
Mourinho aliamua kumfanyia mabadiliko Aurier ambaye alikasirika na anatajwa kuondoka uwanjani wakati wachezaji wenzanke wakiingia kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili na waliokota nyavuni mabao mengine mawili.
Pia inaelezwa kuwa nyota huyo inaweza kuwa ngumu kwake kubaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa amebakiza dili la miezi 18 kumaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo.

Jose Mourinho kuhusu kumtoa beki huyo amesema:-“Ulikuwa ni wakati mgumu na hali ambayo walikuwa nayo wachezaji na ilikuwa ni ngumu kuweza kukubali suala la kupoteza.
“Ni ngumu kukubali hali hasa ya kufungwa mabao ila huwezi kuzuia namna ambavyo inatokea ndani ya uwanja hasa pale ambapo unapata nafasi ndani ya dakika moja. Ni kweli ni hali ya wachezaji hawakuwa na furaha hivyo ni jambo la kawaida,” .
Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!



Caroline
Kawaida Sana…
Sania
Ni kweli kabisa
Adelta
Kawaida
Venerose
Ni kweli kawaida na kama ikitokea hali kama hiyo inatakiwa uongozi uingilie Kati ili kuwaweka wachezaji sawa
Khadija
Kweli kabisa
Sarah
Ni kweli
Lydia Emmanuel Magoti
Mzee wakutoka tusha mzoea
Magdalena
Duh uyu nae anatafuta sababu
Mwanahamisi
Kweli kabisa
Hopemwaikuka
Mbona ndo maisha yetu hayo
Rahmal
Akika ni kweli kabisa
samiah
Kawaida
warda
kweli ni jambo la kawaida