Tetesi zinasema billionea wa Afrika, Aliko Dangote amenukuliwa akisema kwamba ataanza tena harakati za kuinunua klabu ya Arsenal baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 2018.
Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Paris St- Germain Leonardo amesema kwamba ni wakati wa kufanya uamuzi wakati klabu hiyo inapojaribu kukubaliana mkataba mpya na mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Kylian Mbappe.
Tetesi zinasema mazungumzo na mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, yanaendelea vyema kulingana na mkurugenzi huyo wa michezo.

Tetesi zinasema PSG na Inter Milan zina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, atakapokuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu.
Tetesi zinasema beki wa kati wa Torino na Brazil Gleison Bremer, 23, ameonekana kama beki anayelengwa na mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp.
Tetesi zinasema klabu ya Burnley inataka kiasi cha £50m kumuuza kipa Muingereza Nick Pope, 28.
Mshambuliaji wa Uruguay na Inter Milan mwenye umri wa miaka 20 Martin Satriano anasema kwamba anafurahishwa na tetesi zinazomuhusisha na klabu ya Arsenal na Chelsea na angependelea kuhamia katika ligi ya England.
Manchester City inatarajiwa kuwa mshindani mkuu wa Chelsea huku ikijaribu kumsaini mshambuliaji wa Borussia na Norway Erling Braut Haaland, 20, mwisho wa msimu huu.

Manchester United inapanga kuipatia West Ham kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic, 32, au beki Muingereza Phil Jones, 29, katika makubaliano ya kumpata kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice.
Klabu ya Ugiriki ya PAOK huenda inataka kumuuza mchezaji anayelengwa na Man United Christos Tzolis kwa dau la £17m. Winga huyo wa Ugiriki mwenye umri wa miaka 19 amevutia hamu kutoka Barcelona na Borussia Dortmund.
Tetesi zinasema Roma inafikiria kumnunua kwa mkataba wa kudumu kiungo wa kati wa wa Real Madrid Borja Mayora ambaye yuko katika klabu hiyo kwa mkopo.
Tetesi zinasema Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri alikubali kurudi katika klabu ya Stamford Bridge mwezi Januari kabla ya The Blues kumsajili Thomas Tuchel kuwa mrithi wa Frank Lampard.
BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.



Neema juma
Tetesi zimeeleweka hizo
Sadick
Sidhani kama ni muda sahihi kuwekeza kwenye mpira kwa sasa. Dangote anaweza kupteza fedha zake
Rahma
Ziko poa
Adelta
Ziko poa
Angelina
Nice update
Lydia Emmanuel Magoti
Ziko poa
Sarah
Zimesomeka tetesi
Hopemwaikuka
Nmekubalii
warda
Dangote anatisha sana