Manchester United watamenyana na AC Milan katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Uropa, wakati Arsenal wamepangwa na Olympiacos, na Tottenham watachuana na Dinamo Zagreb.
Rangers ya Steven Gerrard lazima imshinde Slavia Prague ili kuongeza muda wa safari zao na Mimaba ya Serie A Roma wanakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Shakhtar Donetsk.
Ratiba ya kusisimua kwenye droo ya 16 bora bila shaka ni mechi ya Manchester United na AC Milan.
Mashindano hayo yatamwona mshambuliaji wa Rossoneri Zlatan Ibrahimovic akikutana tena na klabu yake ya zamani, na Msweden huyo bado anaendelea kuwa na nguvu akiwa na umri wa miaka 39.
Alikuwa sehemu ya kikosi cha mwisho cha Mashetani Wekundu kutwaa kombe hilo, chini ya Jose Mourinho mwaka 2017, lakini hakushiriki katika fainali ya Ligi ya Uropa mwaka huo kwa sababu ya jeraha.
Droo kamili ya 16 Bora ya Europa League.
Ajax vs Young Boys
Dynamo Kyiv vs Villarreal
Roma vs Shakhtar Donetsk
Olympiacos vs Arsenal
Dinamo Zagreb vs Tottenham
Manchester United vs Ac Milan
Slavia Prague vs Rangers
Granada vs Molde
BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.
Ngoja tusubiri dakika90 tuone matokeo
Utakuwa mchezo muhimu kwa Ole na Milan inayotaka kurudi kwenye kilele cha mafanikio
Game kali
Ngoja tuone
Ngoja tuone
Hii si yakukosa
Basi hata hapa United wasituangushe