Saido Yupo Fiti - Yanga

Mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ametolewa kwenye kikosi cha Yanga kitakachomenyana na Kengold FC kwenye mchezo wa michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) kutokana na matatizo ya kifamilia.

Yanga inatarajia kucheza mchezo huo wa ASFC, kesho Jumamosi dhidi ya Kengold FC kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Mchezo wa mwisho kucheza Ntibazonkiza ulikuwa wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC ambapo alifunga bao moja.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka Klabu ya Yanga, kimeeleza kuwa mchezaji huyo alipona majeraha yaliyokuwa yanamsumbua kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Saido alipona majeraha yake lakini kabla ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar aliaga kuwa ana matatizo ya kifamilia hivyo anaenda kwao Burundi.“Aliondoka Jumamosi lakini mpaka leo hajaonekana na hajarejea kikosini hivyo tutamkosa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Daktari ya Yanga, Nahum Muganda alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hana muda mrefu tangu aanze majukumu yake klabuni hapo. Alipotafutwa Ofisa Mhamasishaji, Antonio Nugas hakupatikana.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

7 Komentara

    Nice update

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Good

    Jibu

    Saido tuna kukubali sana mashabiki pole sana na matatizo uliyo nayo

    Jibu

    Inapendeza

    Jibu

    Iko vizuri

    Jibu

    duu ila wachezaji wa hii timu wanaudhuru sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.