Yanga: Bado Tunaimani na Kaze

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kwamba bado una imani na Kocha Mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze licha ya timu kushindwa kupata matokeo chanya ndani ya uwanja kwenye mechi za hivi karibuni.

Yanga mzunguko wa pili imeanza kwa kusuasua huku ikipewa presha kubwa kutoka kwa watani wao jadi Simba ambao kasi yao inazidi kuwa kubwa kila waingiapo ndani ya uwanja.

Mechi ya kwanza waliyocheza dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela waliambulia sare ya kufungana bao 1-1 na walipocheza na Mbeya City ubao ulisoma 1-1.

Pia mchezo wake wa tatu wa mzunguko wa pili ilikubali sare ya kufungana mabao 3-3 jambo ambalo lilipeleka Uongozi wa Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wao Fredrick Mwakalebela kulalamika kwa kusema kuwa  waamuzi wamekuwa wakiwanyima penalti na kutishia kujiweka kando ndani ya ligi.

Mchezo wao uliofuata dhidi ya Mtibwa Sugar, Yanga ilishinda kwa bao 1-0 na kukusanya jumla ya pointi 49 ipo nafasi ya kwanza huku ikifuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na ina pointi 45.

Imeweza kutinga hatua ya 16 bora kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ken Gold mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mshauri wa Yanga kuelekea kwenye suala la mabadiliko, Senzo Mbatha amesema kuwa wanatambua mwendo ulivyo na wana imani na Kaze.

Tunaimani na Kaze na matokeo ambayo tunayapata tunaamini kwamba ni sehemu ya mchezo kwa kuwa ikiwa tutashinda iwe ni kwa mabao mengi ama moja kinachotazamwa ni ushindi.

“Mashabiki wasiwe na presha imani yetu ni kwamba kila kitu kitakuwa sawa na mambo yatakwenda kwenye utaratibu ambao tunahitaji hakuna haja ya kuwa na presha,” .

Machi 4 ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

10 Komentara

    Yanga bado kikosii bora kitafanya vizuri tu

    Jibu

    Yanga bado wako vizuri

    Jibu

    Yanga wako juu

    Jibu

    Kaze yupo vizuri

    Jibu

    Kaze anajua sana

    Jibu

    Kaze namkubali

    Jibu

    wanajipa moyo tu ila hamna kitu

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Mechi ya kwanza waliyocheza dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela waliambulia sare ya kufungana bao 1-1 na walipocheza na Mbeya City ubao ulisoma 1-1

    Jibu

    Mmh

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.