Simba: Aishi Manula Yuko Fiti

Uongozi wa Simba umesema kuwa hali ya kipa namba moja wa timu hiyo Aishi Manula kwa sasa ipo sawa baada ya jana kugongana na mchezaji wa JKT Tanzania, Daniel Lyanga.

Manula aliumia dakika ya 67 baada ya kugongana na Lyanga akiwania mpira ndani ya uwanja ambapo wachezaji wote wawili waliumia ila Manula ilikuwa zaidi kwa kuwa alipoteza pia fahamu na nafasi yake ilichukuliwa na Beno Kakolanya.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ameongea na Manula na amemwambia kwamba yupo sawa isipokuwa anasikia maumivu kwa mbali.

“Aliwahishwa hospitali ya Kairuki na alipewa matibabu na kurejea kwenye hali yake ya kawaida kwa kuwa baada ya kupoteza fahamu aliweza kurejewa na fahamu muda mfupi akiwa ndani ya Ambulace.

“Yassin Gembe, daktari wa Simba ambaye alikuwa na Manula ameniambia kwamba yupo sawa na anaendelea vizuri hivyo anaweza kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Al Merrikh ambapo kikosi kinatarajiwa kuondoka kesho.

“Leo ataruhusiwa na atapewa mapumziko kabla ya kesho kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kujiunga na kikosi kitakachoelekea nchini Sudan,”.

Simba itamenyana na Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi Machi 6.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

11 Komentara

    Manula yuko fiti kweli

    Jibu

    Get well.soon

    Jibu

    Shati la simba

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Mwenyezi Mungu saidia Manula Tanzania one

    Jibu

    Safiii sana

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Safi sana Manula

    Jibu

    Fresh

    Jibu

    Kweli yuko fiti Manula

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.