Tetesi zinasema Real Madrid wako tayari kumuuza Raphael Varane, 27 kwa Manchester United baada ya mchezaji huyo kukataa kusaini mkataba mpya uwanjani Bernabeu.
Gareth Bale, 31 amesema ataishinikiza Real madrid kuheshimu mkataba wake wa £600,000-kwa wiki mpaka utakapomalizika hata kama ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Tetesi zinasema Chelsea bado wanafuatilia kipa wa Italia na AC Milan Gianluigi Donnarumma, 22 na huenda wakamnunua ikiwa hatasaini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Serie A.

Tetesi zimesema kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Jonas Hofmann, 28, amesema kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel anataka kumsajili.
Tetesi zinasema Barcelona na Atletico Madrid wameagizwa kupunguza mishahara kwa kiwango kikubwa kutokana na jinsi janga la corona lilivyoathiri La Liga.
Mgombea urais wa Barcelona Joan Laporta amesema mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi, 33, ataondoka klabu hiyo ikiwa hatashinda uchaguzi wa Machi 7. Mkataba wa sasa wa Messi unamalizika msimu huu.
Tetesi zinasema Dortmund wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Sevilla na Morocco Youssef En-Nesyri, 23, kuchukua nafasi ya Haaland.
Aston Villa hawajaamua ikiwa watampatia mkataba wa kudumu kiungo wa kati wa Chelsea anayechezea klabu hiyo kwa mkopo Ross Barkley, baada ya mkufunzi Dean Smith kutilia shaka thamani ya mchezaji huku Blues wakitaka £35m.

Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Sheffield United Sander Berge,23 ambaye anahusishwa na klabu ya Birmingham amesema mshambuliaji wa zamani wa England Emile Heskey.
Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 22, ana vigezo vyote vya kuwa mchezaji nyota duniani, kwa mujibu wa mchezaji mwenza wa zamani wa Hammers, Sebastien Haller.
Meneja wa Sheffield United Chris Wilder anasema hana huwakika kama ataendelea kukinoa kikosi hicho msimu ujao kutokana na matokeo mabovu yanayoendelea katika timu hiyo.
Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx
Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.



Rahma
Ziko poa
Lydia Emmanuel Magoti
Ziko poa
Sarah
Ziko vizuri tetesi
Adelta
Ziko makini Sana
Venerose
Asanteni kwa taarifa
warda
Acha Varane aje United
Hopemwaikuka
Zmekaa njema
Caroline
Asante kwa taarifa
Angelina
Nice update
Neema juma
Nimezielewa hizo
Mwanahamisi
Ziko poa