Mcheza golf maarufu bwana Tiger Woods amesema anajisikia vyema sana kwa mapokezi aliyoyapata akiwa anarejea mchezoni, Woods anaamini ujio wake mpya umempa mashabiki wengine wapya wengi zaidi kuliko aliokuwa nao mwanzo.
Tiger Woods anarejea baada ya kufanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo zaidi ya mara nne kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu. Tiger Woods, Mmarekani mwenye umri wa miaka 42 kwa sasa yuko kwenye mjadala wa Ryder Cup, anaamini mashabiki wanamapenzi ya dhati na yeye hasa kutokana na ujio wake mpya. Tiger Woods anadai “watu wanatambua kuwa ninakaribia mwisho kutumikia mchezo huu, japokuwa sitambui siku ngapi zimebaki lakini naweza tambua kuwa Tiger Woods nilivyo katika umri wa miaka 22 sio Tiger Woods huyu mwenuye miaka 42.
wiki hii Tiger Woods atakuwa uwanjani pale New Jersey katika kombe la FedEx Cup , kwa maneno yake anasisitiza kuwa haijawa rahisi kurudi baada ya kufanyiwa upasuaji mara 4 lakini anaamini mashabiki wake wanaelewa hilo na atajitahidi kufanya vizuri.


Povel
Gud news