Winga wa Everton, Ademola Lookman anaripotiwa kuwa ameshaandaliwa kuondoka Everton kujiunga na RP Leipzig. Taarifa hizi zimeripotiwa na chanzo cha habari cha The Mirror kuwa tayari mchezaji huyu yuko mbioni kuondoka Everton na tayari alikuwa ametemwa kwenye kikosi ili kujiandaa kuondoka.
Ademola Lookman alijiunga everton mwaka 2017 akiwa anatokea Charton Athletic na akawa anafukuziwa na RB Leipzig kipindi chote cha majira ya joto na sasa inaonekana dili inakaribia kutiki baada ya RB Leipzig kuripotiwa wanacheza na ofa ya Euro milioni 25 kwa winga huyo.
Meneja wa Everton, Marco Silva angehitaji kumbakiza kijana huyo, amesikika akisema kijana huyo ni muhimu kwa kesho ya Klabu. Lookman mwenyewe hajasikika hadharani akizungumzia sana kuhusu uwezekano wake wa kuondoka Everton. Lakini wadau wanasema ukitazama dili hili kibiashara zaidi, basi Everton watatengeneza faida kubwa kwa kuwa wao walilipia euro milioni 11 kwa Ademola Lookman, lakini kwa upande mwingine wako mbioni kumpoteza mchezaji mwenye kipaji.


Sadick
Anaenda kuziba gap la Timo Werner#meridianbettz
Povel
Look man yupo vzr sana abaki apate huzoefu tu