Aliyewahi kuwa mchezaji wa Arsenal Alan Smith amesema kwa sasa Arsenal hawahitaji kushinda ubingwa, inahitaji tu mabadiliko chanya. Alan Smith amesema hayo kufuatia washika mtutu hao kuanza vibaya msimu wakiwa na meneja wao mpya Unai Emery. Bwana Emery ambaye amepokea kijiti kutoka kwa Arsene Wenger anataniwa kuwa amepata ubatizo wa moto katika kippindi cha kwanza cha kuanza kutekeleza majukumu yake hapo Arsernal baada ya kucheza na Manchester City na Chelsea.
Allan Smith anasema kwa sasa anafikiria arsenal inapaswa kupiga hatua kuwa licha ya kuwa na mwanzo mbaya. Yeye anadai yuko tayari kuwa na subira kuona mabadiliko katika kipindi hiki ambacho Unai Emery anaanza kazi, anatoa wito kwa wadau wengine wa washika bunduki hao kuwa na subira na kusubiri matunda mema ya shughuli ya Unai Emry. Alan Smith anasisitiza kwamba angalau angependa kuona arsenal wanamaliza katika nafasi 4 za juu sio lazima wachukue Kombe.


Issa
The gunners wanashida ya ndoo
Gabriel
Arsenal jeshiii