Arsernal wa Unai Emery leo anamkaribisha West Ham United pale Emirates Stadium. Washika mtutu na washika nyundo wote wana njaa ya kupata pointi leo baada ya kuanza vibaya. Je nani mbabe leo? ni mwenyeji Arsenal au wageni West Ham United, hapa ipo rekodi na taarifa ya wakali hawa wanaomenyana leo inayoweza kuongoza utabiri wa nani anaweza kumbetua mwenzake pale Emirates.
Wakali hawa wanaingia uwanjani leo wakiwa wanarekodi zinazofanana katika jumla ya mechi 6 walizocheza hivi karibuni. Arsenal amepoteza 2, Ameshinda 2, ametoa sare 2. wakati huo West Ham amepoteza 2, ameshinda 2, na ametoa sare 2 pia. Katika jumla ya gemu 44 ambazo mshika mtutu amekutana na West Ham United kwenye Primier League, Arsernal amefanikiwa kumdunda West Ham mara 28 wakati West Ham akiambulia kumpiga Arsenal mara 7 tu. Gemu ya leo inakuwa ni ya 139 kwa timu hizi kukutana uso kwa uso, huku Arsenal akishinda mara 65 na West Ham mara 34. Mengine yanayotarajiwa leo kwa vikosi na mifumo yapo hapa;
Arsenal
Mfumo : (4-2-3-1)
Kikosi : Cech; Bellerin, Mustafi, Sokratis, Monreal; Guendouzi, Torreira; Mkhitaryan, Ozil, Lacazette; Aubameyang
Majeruhi : Koscielny , Kolasinac , Maitland-Niles, Jenkinson
West Ham United
Mfumo : (4-2-3-1).
Kikosi : Fabianski; Zabaleta, Balbuena, Ogbonna, Masuaku; Wilshere, Noble; Snodgrass, Felipe Anderson, Arnautovic; Hernandez
Majeruhi: Reid, Lanzini , Carroll.


Furahav
Arsenal hii haiko vizuri,itafungwa tu.
Povel
Hapo gg tu
Njiku
Mechi ngumu sana ila ngoja tuone