Sarri: "Nina Deni Kubwa kwa Benitez"

Bosi wa Chelsea, Maurizio Sarri anasema anadaiwa deni kubwa la fadhila kwa Rafael Benitezi wa New Castle United. Bosi huyu aliipotea timu ya Napoli kutoka katika mikono ya Benitez mwaka 2015 na kuwafikisha nafasi ya pili nyuma ya Juventus. anasema ni mafanikio ya napoli yaliyomfanya aonekane na mpaka sasa kuwa Chelsea anaamini ni mafanikio hayo yalimpa nafasi. Newcastle United wanawakaribisha Chelsea jumamosi ya leo tarehe 25, Augosti 2018.

Maurizio Sarri mwenye umri wa miaka 59, aliungana na Chelsea Julai !4, 2018 na anatarajiwa kuwepo chelsea hadi Juni 2021. Sarri anasema mtangulizi wake alitengeneza mazingira ambayo yalimrahisishia yeye kupata ushindi akiwa na Napoli. Kwa maneno yake anadai, “Benitez alitengeneza msingi, Lazima nimshukuru…. nilipofika nikahisi timu tayari imeshandaliwa kucheza soka kwa staili yangu.”  Maurizio Sarri anakiri kuwa atakuwa na mchezo mgumu anavyokutana na Newcastle United, anasema kuwa ni wapinzani hatari sana na wana kocha mzuri. Sarri anasisitiza kuwa wanazoezi gumu sana kwa Newcastle United kuwa msimu uliopita walipoteza 3-0, laikini sio wao tu, hata Manchester United na Arsenal walifungwa pia.

3 Komentara

    Safi

    Jibu

    Ha bar njema

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe