Winga wa Everton Yannick Bolasie amejiunga Aston Villa kwa mkopo msimu mzima. Bolasie amekuwa mchezaji wa 4 kwa Aston Villa kusajiliwa kwa mkopo baada ya kuwasajili wengine wa 3 ambao ni Andre Moreira, Axel Tuanzebe na Anwar El Ghazi wakati Orjan Nyland na John McGinn wakisajiliwa kwa mikataba ya kudumu.
Mwanzo ripoti zilionyesha Yannick Bolasie alikuwa akihitajika kwa mkopo na Middlesbrough, lakini Villa wanawapiga gepu kwa kumchukua staa huyu. Bolasie alijiunga Evarton kwa ada ya Euro milioni 25 mwaka 2016, amewafungia magoli 2 katika michezo 34. Disemba 2016 alipata jeraha la goti lililomfanya awepo nje kwa mwaka mzima hadi kipindi cha Boxing day Disemba 2017 aliporejea dimbani.
Bolasie anafurahia uwepo wake Aston Villa, kupitia picha ya video iliyopostiwa katika mtandao wa Yutube ameonyesha hisia zake juu ya kujiunga na timu hiyo. “Niko hapa kujipa tabasamu tena na kutumia uwezo wangu kujaribu kuisaidia timu. Nafurahi sana kuwa hapa” amesema staa huyu.


Fatina mfingi
Asnteh kwa taarifa meridianbet