Arsenal Atachomoka Leo?

Arsernal wa Unai Emery leo anamkaribisha West Ham United pale Emirates Stadium. Washika mtutu na washika nyundo wote wana njaa ya kupata pointi leo baada ya kuanza vibaya. Je nani mbabe leo? ni mwenyeji Arsenal au wageni West Ham United, hapa ipo rekodi na taarifa ya wakali hawa wanaomenyana leo inayoweza kuongoza utabiri wa nani anaweza kumbetua mwenzake pale Emirates.

Wakali hawa wanaingia uwanjani leo wakiwa wanarekodi zinazofanana katika jumla ya mechi 6 walizocheza hivi karibuni. Arsenal amepoteza 2, Ameshinda 2, ametoa sare 2. wakati huo West Ham amepoteza 2, ameshinda 2, na ametoa sare 2 pia.  Katika jumla ya gemu 44 ambazo mshika mtutu amekutana na West Ham United kwenye Primier League, Arsernal amefanikiwa kumdunda West Ham mara 28 wakati West Ham akiambulia kumpiga Arsenal mara 7 tu. Gemu ya leo inakuwa ni ya 139 kwa timu hizi kukutana uso kwa uso, huku Arsenal akishinda mara 65 na West Ham mara 34. Mengine yanayotarajiwa leo kwa vikosi na mifumo yapo hapa;

Arsenal

Mfumo : (4-2-3-1)

Kikosi : Cech; Bellerin, Mustafi, Sokratis, Monreal; Guendouzi, Torreira; Mkhitaryan, Ozil, Lacazette; Aubameyang

Majeruhi : Koscielny , Kolasinac , Maitland-Niles, Jenkinson

West Ham United

Mfumo : (4-2-3-1).

Kikosi : Fabianski; Zabaleta, Balbuena, Ogbonna, Masuaku; Wilshere, Noble; Snodgrass, Felipe Anderson, Arnautovic; Hernandez

Majeruhi: Reid, Lanzini , Carroll.

3 Komentara

    Arsenal hii haiko vizuri,itafungwa tu.

    Jibu

    Hapo gg tu

    Jibu

    Mechi ngumu sana ila ngoja tuone

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.