Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Massau Bwire amekiri timu yake kufanya vibaya katika mechi kadhaa zilizopita huku akidai watafanya mapinduzi dhidi ya Yanga SC.
“Kumekuwepo na upepo mchafu hapa katikati uliopita ambao hata sisi hatujui umekujaje na umetokea wapi, ambao kwa kiasi flani ulipunguza ile kasi yetu na matarajio yetu, ambapo baadhi ya watu walifikiria ule ndio uwezo wetu umeishia pale” alianza Bwire.
“Lakini kupitia mchezo wa kesho dhidi ya Yanga SC tunahitaji watu waendelee kutuamini na kujua hii ndio Ruvu Shooting halisi na ndio maana ikaitwa Barcelona ya bongo”
“Mimi naomba niwaambie Yanga waje na tahadhari hasa mashabiki wale wanaokuja na Matokeo yao kuwa iwe isiwe lazima wachukue pointi 3 kwa Ruvu Shooting, mimi niwaambie ni Jambo ambalo halitawezekana na wasije wakaisumbua red cross mara mtu amepeleka macho juu, mara mtu ameanguka na kupoteza fahamu sababu tu ya kile walichokitarajia hakikuwa ivo”
“Mimi naomba waje wakijua chochote kile kinaweza kutokea na siyo mtu anakuja na matokeo yake mkononi sijui mwingine anakuja na matokeo kichwani”
“Tunao uwezo mkubwa sana sasa hivi katika kucheza mpira, na kesho PTK inaenda kurudisha makali yake, tunaenda kuwahudumia yanga PTK kwa maana ya Papasa Tingisha Kunguta, ili Yanga waende kumaliza ligi wakiwa wanafahamu Kuna kitu kinaitwa PTK na hao PTK hawakuwa na utani hivyo tunaenda kuyashuhudia kesho,” aliongeza Bwire
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑


