Ni siku 22 tu zimepita tangu Gennaro Gattuso kukabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi cha Fiorentina. Kimeshaumana huko Italia.
Imeripotiwa kuwa Gattuso na uongozi wa Fiorentina umepishana kwenye malengo ya usajili majira haya ya joto. Kabla ya kocha huyo kuchukua nafasi hiyo, aliitaka klabu hiyo kumuhakikishia usajili wa Sergio Oliveira (FC Porto) na Goncalo Guedes (Valencia). Mambo yamekuwa tofauti.
Uhalisia ni kuwa, hakuna njia nyingine ya kusuluhisha mgogoro huu na uongozi wa Fiorentina unaangalia namna sahihi ya kusitisha mkataba wa kocha huyo kisheria.
Tayari baadhi ya makocha wameanza kufikiriwa kama mbadala wa Gattuso, kati yao ni Rudi Garcia na Claudio Ranieri
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑


