Mmiliki wa Klabu ya The Bluez, Roman Abramovich anaamini klabu ya Borussia Dortmund itamruhusu Haaland kujiunga na Chelsea majira haya ya kiangazi.

Kwamujibu wa taarifa kutoka Uingereza zimebainisha kuwa Abramovich amesema ni matumaini yake kuwa klabu hiyo ya ujerumani itamuachia Haaland kujiunga na Chelsea, mazungumzo ya pande hizo mbili yanaendelea ili kukamilisha mpango wa Haaland kutua Darajani.
Chelsea wameweka nguvu zao Kwa Haaland mara baada ya mchakato wa kumpata Harry kane na Romelu Lukaku kuonekana Kuwa na vikwazo vingi.
Chelsea watarajia kupata upinzani mkubwa kutoka Kwa Real Madrid, Bayern Munich na Manchester city ambao wote wameonesha dhamira ya kutaka kumsajili kinda huyo wa Dortmund.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

