Liverpool Watalipa £60m kwa Nicolo Barella?

Liverpool wanatajwa kuwa wana andaa ofa ya pesa nyingi kwa ajili ya kiungo wa Inter Milan Nicolo Barella.

Mchezaji huyo wa miaka 24, ambaye alikuwa na mchango kwenye mafanikio ya timu yake ya taifa Italia kwnye Euro 2020, alifunga mara tatu na kutoa asisti 13 katika mechi 46 za Inter Milan kwenye kampeni ya 2020-21.

Barella bado amebakiza miaka mitatu kwenye mkataba wake huko San Siro, lakini ripoti ya hivi karibuni ilidai kwamba Liverpool waliwasiliana na Inter kuzungumzia juu ya uwezekano wa uhamisho wakati wa msimu huu wa usajili wa majira ya joto.

Liverpool Watalipa £60m kwa Nicolo Barella?

Kwa mujibu wa La Repubblica, Liverpool sasa wanaandaa zabuni kumnasa Muitaliano huyo, ambaye anasemekana anathaminiwa na mabingwa wa Serie A kwa pauni milioni 60.

Inter iko chini ya shinikizo ya kuuza wachezaji wao muhimu msimu huu wa joto kutokana na shida za kifedha, ingawa inafahamika kuwa klabu inaandaa mpango mpya na Barella.

Kiungo huyo, ambaye alifunga mara moja na kutoa asisti mbili katika safari sita za Euro 2020, amefunga mara saba na kusajili asisti 21 katika mechi 87 kwa timu yake ya sasa kwenye mashindano yote.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.