Ni hali ya kushtua kuona Lionel Messi anaondoka Barcelona ikiwa ni muda mfupi tangu kuripotiwa makubaliano ya mkataba mpya na klabu hiyo.
Messi amemaliza mkataba wake wa awali na Barca toka Juni 30,2021 lakini maongezi ya mkataba mpya yalikuwa yakiendelea na mpaka dakika za mwisho (kabla ya taarifa ya kuondoka kwake), mchezaji huyu alikuwa anabaki Camp Nou.
Alhamisi usiku, mambo yakabadilika. Ulimwengu wa soka ukazizima pale FC Barcelona (kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii) kuripoti kuwa hawatoweza kuendelea na nahodha wao licha ya kuwa na makubaliano ya kusaini mkataba mpya wa miaka 5.
Ni mengi yanasemwa na kila mmoja akiwa katika sintofahamu. Raisi wa Barcelona, Joan Laporta amezungumza na waandishi wa habari kufuatia kilichotokea kwenye mchakato mzima.

Akizungumza na waandishi wa habari, Joan Laporta anasema;
“Tulikuwa na makubaliano na Messi ya mkataba wa miaka 5 lakini tungemlipa mshahara wa miaka 2. Leo alikubali mkataba, kila kitu kilikubaliwa. Tuliamini tupo sahihi kwenye kipengele cha usawa wa kiuchumi (Financial Fair Play) lakini, haikukubaliwa na LaLiga.
“Ninahuzuni kwasababu tulifanya kila tuliloweza ili kumbakiza Leo,na yeye pia alikuwa tayari kubaki Barcelona, tulishakubaliana. Lakini sasa yanaanza maisha mapya bila Leo, tutaendelea kumshukuru daima.
“Nafasi ya kubadilisha hali ilivyo na kumsajili tena Messi? Sitaki kutoa matumaini ya uongo.Tulikuwa na muda wa kushughulikia hili, LaLiga inaanza wiki ijayo, sasa hivi Leo anaweza kuangalia timu zingine.”
Hakika ni huzuni kumpoteza mchezaji aliyeitumikia klabu yake kwa miaka 21 akitwaa mataji 10 ya LaLiga, 4 ya Ligi ya Mabingwa na tuzo 6 za mchezaji bora wa dunia.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!



Sania+mapua
Messi wacha aende tu