Kocha msaidizi wa Simba SC, Mrwanda Thierry Hitimana ameiomba radhi Klabu ya Mtibwa Sugar kwa kile kilichotokea baina yake na viongozi wa timu hiyo.

“Kila kitu waligharamia wao mpaka nafika nchini ila baada ya kuanza mazoezi nao nikapigiwa simu na mabosi wa Simba SC wakinihitaji nikafanye kazi na Gomes, nikakubaliana nao kwa sababu ni mtu ambaye tumewahi kufanya kazi pamoja tukiwa Rayon Sports.
“Mtibwa Wana rasilimali nzuri ya wachezaji hivyo naamini kocha atakayekuja atafurahia na kufanya vizuri zaidi kwenye Ligi,” alisema Hitimana huku akiwaomba yaishe wafungue ukurasa mpya kwani Mtibwa ni nyumbani kwake.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtibwa Sugar, Nassoro Abubakar alisema wamemsamehe kocha huyo huku wakimtakia kila la heri katika maisha yake mapya.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


