Tetesi zinasema, Manchester United bado wameonesha utayari wa kupata saini ya mchezaji wa Borussia Dortumund na raia wa Norway kiungo Erling Braut Haaland, licha ya kurudi mchezaji machachari raia wa Ureno Cristiano Ronaldo,36.
Tetesi zinasema, Lionel Messi, 34, atapata £25.6m katika misimu miwili ijayo akiwa na Paris St-Germain, Mchezaji huyo raia wa Argentina mshahara wake unatarajiwa kuongezeka zaidi mpaka kufikia £8.5m katika kipindi cha miaka mitatu.
Wakala wa mchezaji Matthijs de Ligt, Mino Raiola anasema kuwa beki huyo wa kati wa Uholanzi anaweza kuondoka Juventus mwishoni mwa msimu, huku Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 22.

Kocha msaidizi wa West Ham United Kevin Nolan anasema kuwa hana mpango wowote wa kumuachilia Declan Rice,22,-huku kipaumbele chake zaidi kikiwa ni kuwapatia Manchester United kwa £100m.
Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Manchester United, Edinson Cavan ameonesha nia yake ya kusalia Old Trafford licha ya kwamba mchezaji huyo raia wa Uruguay kugombania namba na Ronaldo.
Chelsea imeonesha nia ya kutoa ofa nzuri kwa kiungo wa Monaco Aurelien Tchouameni,21, kujiunga na Stanford Bridge, huku Juventus nao wameonekana kuvutiwa na mchezaji huyo raia wa ufaransa.
Bosi wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekubali kwamba bado hajaamua mlinda mlango yupi atakuwa chaguo lake la kwanza msimu huu, kati ya David de Gea 30 wa Uhispania na Dean Henderson, 24 wa Uingereza.

Mlinzi wa Aston Villa, Matty Cash anatakiwa na Poland kabla ya raundi inayofuata ya kufuzu Kombe la Dunia kwa sababu mchezaji huyo wa miaka 24 ameonesha utayari wake wa kuchezea nchi ya upande wa mama yake.
Tetesi zinasema, Kocha wa Wolverhampton Wanderers, Bruno Lage amevionya vilabu vya Manchester United na Arsenal kuwa hatamruhusu kiungo wa Ureno Ruben Neves, 24, aondoke bila ya kumaliza michezo yake.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!



Sarah
Ziko poa tetesi