Barcelona wameanza kuwachokonoa Chelsea kwa kuonesha nia ya kutaka kumsajili Willian kikosini mwao. Ripoti hizo za mchezaji huyo kuanza kuhusishwa na klabu hiyo zimeibua sura mpya hii ni baada ya kuanza kuhisiwa kwamba inawezekana Coutinho asiwe na nafasi tena kuendelea kusalia kikosini hapo; baada ya kuona labda hawezi kuendana na mfumo wa mwalimu na mahitaji ya mwalimu katika kikosi hicho. Barcelona sasa, kwa hatua hiyo watasajili majina mengi makubwa ndani ya kikosi hicho na hali hii kisoka inadumaza ushindani kwa kiwango kikubwa. Wao wameweka mezani kiwango cha A$89M, na kuweza kumuondoa aidha Malcom au Coutinho anaeonekana kutofurahia kikosini hapo.
Safari ya Ramsey [28] inaonekana kuiva zaidi kuelekea kujiunga na wababe wa Serie A: Juventus. Ikiwa kandarasi yake kuendelea kusalia klabuni hapo inaelekea ukingoni, mchezaji huyo amekwisha fanya maamzi ya awali na kujadili juu ya kutimkia katika klabu hiyo mapema msimu ujao. Pamoja na maamzi hayo, kocha Emery ataruhusiwa kuendelea kumtumia mchezaji huyo hadi msimu ujao. Kilichobaki hadi sasa ni makubaliano ya kimalipo kati ya klabu hizo mbili; ili mchezaji huyo aweze kujiunga rasmi na upande huo wa Juventus kwa sasa.
Manchester United kukinga kibubu endapo Mourinho atasaini kuifundisha Madrid, ikiwa Mreno huyo atafanikiwa kupata kibarua hicho ndani na jiji la Hispania; Madrid watakuwa wakimlipa Man United kiwango cha $18M. Hii ni baada ya makubaliano ya mkataba uliowahi kusainiwa kati klabu na Mourinho 2016 kwamba endapo ataondoka klabuni hapo kabla ya mkataba wake kuisha, atakuwa huru kujiunga na klabu yoyote ila klabu hiyo itatakiwa kulipa fidia ya kiasi fulani kutokana na matumizi yake. Hii ndiyo inaitwa biashara ya akili ambayo Ed Woodward aliiweka wazi mwanzoni kabisa aliposainishana mkataba na mwalimu huyo. Madrid wanaonekana kutaka kumrejesha kwa mara ya pili kocha huyo katika klabu yao hiyo.
Michy Batshuayi anatafutwa na klabu nyingi kubwa Uingereza, akiwa bado ni mchezaji wa Chelsea; ameanza kutolewa macho na klabu mbalimbali nchini Uingereza ili aweze kutoa msaada katika safu zao za ushambuliaji. Mchezaji huyu alikuwa anepelekwa Valencia na amehudumu kwa mkopo ndani ya klabu hiyo, lakini wakati wake wa kuendekea kusalia klabuni hapo kwa mkopo umefika kikomo. Kwa sasa anatakiwq kurejea darajani kuungana na timu yake. Lakini, klabu kama Everton zinamfukuzia baada ya wachezaji wake Cenk Tosun na Dominic Calvert-Lewin kuonekana wanapata tatizo kuendana na kasi ya timu hiyo.
Fulham bado wana matumaini ya kumnasa Cahill, klabu hoyo bado haijakata tamaa kuendelea kufukuzia saini ya mkongwe huyo wa Chelsea ili waweze kumpata. Wamekuwa wakihusishwa mara kwa mara na kumsajili mchezaji huyo ili aweze kufanya kazi ya kuisaidia timu hiyo kufika hatua kubwa ambapo wanaamini kuwepo kwa wakongwe kama hawa ndani ya klabu yao kutakuwa na manufaa makubwa.



Furahav
Na baka wanaweza kumchukua.
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa