Mouriho: Heshima Kubwa Kuhusishwa na Vilabu Hivi

Aliyekuwa meneja wa Manchester United, Jose Mourimho anaendelea kuteka vichwa vingi vya habari licha ya kutokuwa na kibarua chochote kwa sasa. Mourinho anatawala vichwa kwa kuhusishwa na klabu mbalimbali zikiwemo zile ambazo tayari ameshawahi kuzitumikia kipindi cha nyuma.

Mourinho anasema kwake ni heshima sana kuhusishwa na vilabu ambavyo alikuwa akivitumikia vipindi vya nyuma. Kwake hilo ni suala la kujivunia kwa sababu ni wazi inadhihirisha mchango aliokuwa nao kwenye vilabu hivyo.

Baadhi ya vilabu ambavyo meneja huyu amekuwa akihusihwa navyo ni pamoja na Inter Milan, Real madrid. Benifica pia walimuomba meneja huyu ili awe meneja wao baada ya kumtimua aliyekuwa meneja wao wiki kadhaa zilizopita.

“Kama mchezaji au meneja anahitajika na klabu yake ya mwanzo, inamaanisha alitoa mchango chanya kwa klabu hiyo. Mjuzi akirejea kwenye klabu ni heshima kubwa mno, wanakuwa hawamchukui mtu mgeni kwao, wanakuwa wanamchukua mtu wanayemfahamu vyema zaidi.” -Mourinho

Mourinho alikuwepo kwa misimu miwili klabu ya Inter Milan, baada kutoka Chelsea mwaka 2008 akishinda mataji 2 ya Serie A na kutwaa Ubingwa wa Ulaya. Mwaka 2010 alienda Real madrid akiwatumikia kwa miaka 3 na kuwaaacha na taji moja la La Liga.

3 Komentara

    Ni kocha mzuri sana

    Jibu

    Kocha mzuri

    Jibu

    Mambo moto moto

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.