Isco amekuwa na wakati mgumu siku za hivi karibuni, anapitia kipindi cha kutopewa nafasi sana kwenye kikosi cha Santiago Solari pale Real Madrid, katika gemu 3 zilizopita nyota huyu aliingingia kama sabu wakati akipata nafasi ya kuanza kwenye gemu moja tu tokea Santiago Solari alipochukua kibarua klabuni hapo.
Madrid wanaenda kwenye gemu dhidi ya Real Betis jumapili wakiwa wametoka kupokea kichapo cha 0-2 dhidi ya Real Sociedad kwenye dimba la Santiago Bernabeu wiki iliyopita. Solari naonekana bado haypo tayari kumpa nafasi Isco kwenye kikosi chake cha kwanza .
Kwa mujibu wa Solari, anadai anapata wakati mgumu wakati wa kupanga kikosi nani aanze au nani akae benchi, Isco ni kama wachezaji wengine na anacheza vizuri lakini yeye ndiye anatambua nini anatakiwa kufanya ili aweze kwenda sawa na meneja huyu wa sasa wa klabu hii.
Wakati huo, klabu hii inaripotiwa kuwa Real wanamuhitaji Dyabala kutoka Juventus kwa kufanya dili la kubadilishana wachezaji na klabu hiyo.
Ataenda Juve?

Real wanadaiwa kuwa wanataka wampate Dyabala kwa kubadilishana na Isco. Lakini wawili hawa wanaripotiwa kuwa uhamisho wao una thamani inayopishana kidogo, wakati Isco akiwa na dau la paundi milioni 80, dau la Paul Dyabala ni paundi milioni 100.
Kama Juventus watakuwa na uhitaji na nyota huyu huenda wakampa nafasi ya kupata mda zaidi wa kupiga soka tofauti na mda ambao amekuwa akiupata Chini ya Solari. Lakini, bado Juventus sio rahisi sana kumpoteza kinda paul Dabala kwa wakati huu licha ya kuwa na Mafundi wengine kama Cristiano Ronaldo. Bila shaka dili hili ni gumu kwa Juventus lakini linawezekana.


Furahav
Apambane tu.
Njiku
Isco kapotea sana kwenye game hatusikii mambo yake wala hatuoni vitu vyake uwanjani,paul dybala kinda ambaye anaekipiga juventusi yupo sanaa na sidhani juventus watakubali ofa hiyo wanaotaka kupewa na real madrid.hii ni danganya toto kupewa mchezaji aliyepotea na kuchukua dhahabu