Kuhusu Usajili Jumapili Hii!

Hapa tunakuletea stori kuhusu usajili Jumapili hii. Hapa zipo zile zinazosemwa hadharani na vilabu husika, makocha, wachezaji na mawakala wao. Lakini pia zipo zile za nyuma ya pazia ambazo bado!

Philipe Continho ameingia kwenye vichwa vya habari akionekana kuwa mbioni kusepa Barcelona na kuhuzishwa na Manchester United . Ni mwaka mmoja tu tangia staa huyu alipoingia Barcelona, hata hivyo staa huyu amekuwa akikumbana na kipingi kigumu katika kupata gemu klanuni hapo. mpango wake unadaiwa ni kwenda Man utd ambao wanaripotiwa kuwa walikuwa wanamfukuzia siku za hivi karibuni.

Kuhusu Usajili Jumapili Hii!
Denis Suarez

Arsenal wanaripotiwa kuwa wataonana na Barcelona Jumatatu ya kesho ili kujadili kuhusu Denis Suarez kama wanaweza kumchukua nyota huyu kwa mkopo. Nyota huyu amekuwa akitupiwa jicho zaidi na Arsenal kipindi cha hivi karibuni huku bosi Unai Emery akisema dili la mkopo ndiyo kinachoweza kufanyika kwa usajili wa dirisha hili. Suarez anaripotiwa kuwa kwa nafasi yake Barcelona haitakuwa ishu ya kushangaza sana kama Barcelona wakimuacha ende Man Utd kwa Mkopo.

Kuhusu Usajili Jumapili Hii!
Aaron Ramsey

 

 

 

Aaron Ramsey naye anaripotiwa kuwa leo atakuwa kwenye vipimo tayari kuungana na klabu hii baada ya kubaniwa mkataba mwingine klabuni Arsenal. Kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport maafisa wa Juventus watatua jijini London kwa ajili ya vipimo vya nyota huyu.

Bournemouth wanaripotiwa kuwa wanajiandaa kumpatia mkataba mpya nyota wa klabu bhiyo David Brooks. Tokea alipofika klabuni hapo kutokea Sheffield, nyota huyu amekuwa akiwavutia klabu mbalimbali huku Manchester United na na Tottenham Hotspurs wakiripotiwa kumfuatilia maendeleo yake klabuni hapo.

Pep Guardiola anadai kuwa yeye hana mpango wa kuongeza kikosi chake cha Man City mwezi huu. Guardiola anadai kuwa yeye anaridhika na kikosi chake, labda angekuwa na majeruhi ambao wangemlazimu kuongeza kikosi kwa wakati huu. Ila kwa kipindi hiki anajiona yupo gado kuendelea na wachezaji alioanza nao msimu.

Kuhusu Usajili Jumapili Hii!
Guardiola

Bayern Munich wanadaiwa kuwa wanataraji kukaa meza moja na Chelsea kuangalia uwezekano wa kumsainisha Alvaro Morata ambaye kwa sasa anaonekana anahitaji kusepa klabuni hapo baada ya kuonekana hapati nafasi sana kwenye kikosi cha Sarri.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.