Imani ni kitu ambacho kipo nafsini mwa mtu mwenyewe, na hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mwingine afanye kitu kingine bila hiari yake. Katika soka pia haya mambo yapo; mchezaji anayeamini katika upande fulani anaweza kuachana na upande ule na baadaye akajiunga na upande mwingine. Leo tutaonyesha baadhi ya wanamichezo wakubwa na wenye historia zao waliopata kuzihama dini zao. Zipo sababu mbalimbali zilizomfanya mtu ahame kutoka dini moja kwenda nyingine. Hapa watazungumziwa walioacha uislamu na kuamini katika ukristo.
George Weah – Liberia, alizaliwa mwaka 1966 na akafanikiwa sana katika soka la kulipwa ambapo alifanikiwa kuchezea vilabu vingi vikubwa kama Monaco, AC Milan na Chelsea. Mwaka 1995 alitajwa kuwa mchezaji bora wa FIFA na kujinyakulia tuzo kwa hatua hiyo kubwa; pia katika bara la Afrika amejenga historia kubwa ambayo bado inaishi hadi sasa. Weah alikuwa Muislamu, lakini alikuja kufanya maamzi ya kuchana na dini hiyo akitaka kumjua zaidi Yesu Kristo na kufuata nyayo zake. Hakuishia hapo baada ya kukaa miaka kadhaa aliamua kurudi tena kwenye dini ya Kiislamu. Lakini, baada ya kumuonja Kristo akaamua kuhitimisha safari yake ya kuuvaa ukristo.
Djibril Cissé – Ufaransa, alizaliwa mwaka 1981 ambapo wazazi wake walihamia nchini humo kutoka Ivory coast. Alianza kujihusisha na soka akiwa na miaka nane tu, huku akifanikiwa kung’ara kwenye klabu nyingi kubwa ambazo ni Auxerre, Liverpool, Marseille, Sunderland, Panathinaikos, Lazio na Queens Park Rangers. Na ilipofika mwaka 2007, aliweza kubadili dini yake ya Kiislamu huku akijiunga na Ukirsto. Lakini nyuma kidogo mwaka 2005 aliweza kufunga ndoa na Jude Litter ambaye alikuwa ni mkristo. Hivyo, mwanamke huyo ametoa ushawihi mkubwa katika kuihama dini kwa mchezaji huyo.
Kabeer Gbaja-Biamila – Marekani, alizaliwa mwaka 1977 huku familia yake wakiwa na misingi ya kiislamu wakihamia ndani ya taifa hilo kutoka Nigeria. Jina lake Gbaja-Biamil lina maana ya “mwenye uwezo fanya unisaidie”. Ana historia chanya katika soka ikiwa ni pale alipoichezea Green Bay Packers. Pamoja na maneno ya chuki aliyopenyezewa na baba yake juu ya ukristo, aliweza kupingana nao na kuanza kutumia muda wake mwingi kusoma vitabu vinavyohusishwa Ukristo. Na hadi kufikia 2000 alikuwa amekwisha kujiunga na ukristo.
Tunch Ilkin – Uturuki, alizaliwa mwaka 1957 huko Instanbul. Aliweza kuhamia Chicago na familia yao akiwa na umri wa miaka miwili. Aliweza kuachana na soka na kujiunga na NFL huku akiwa kama Makamu wa Raisi wa bodi hiyo. Baadaye aliweza kujiunga na ukristo kwa kuridhishwa na matendo yao. Kwa sasa ni mchungaji na anahudimu katika kanisa lake alilolianzisha linaloitwa Men’s Ministry at Bible Chapel hukohuko Marekani.


Povel
Kwl first mungu