Hii ni katika hatua ya makundi ambapo kila timu inapigana kujikusanyia alama ili iweze kujiweka mahala pazuri kuweza kusonga mbele. Simba akiwa kinara wa kundi hilo kwa kuwafunga Waalgeria; sasa anarejea upya kwenda kukutana na vigogo wa Kongo ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya michuano hiyo mikubwa Afrika.
Wapinzani ahao wa Simba wamejaribu kuangalia kadi waliyo nayo wapinzani wao na kuongeza uwezo wa kikosi vhak hasa katika safu ya ulinzi kwa kumshusha mchezaji kinda mpya katika klabu hiyo ili waweze kumudu kasi ya washambuliaji wa klabu ya Simba. Mchezaji huyo ni Savio Kabugo ambaye wamemshusha katika kikosi chao kitakachokabiliana na simba.
Imeripotiwa kwamba klabu hiyo inaandaa mipango kabambe ya kuwazuia Simba kuondoka na alama yoyote ndani ya ardhi yao; na lengo kubwa la kumshusha mchezaji huyo ni imani yao kwamba; kwa sababu huyo ni mchezaji mwenye asili ya Afrika mashariki, atakuwa anajua mbinu nyingi zinazotumiwa na wachezaji wenza wa Afrika Mashariki. Kwa kufanya hivyo wanaamini hiyo kama njia pekee ya kukabiliana na mpinzani wao.
Safu ya ushambuliaji ya Simba imekuwa mwiba mkali kwenye michuano hiyo mikubwa kwa kuwa na uwiano mzuri wa magoli. Safu yao imekuwa ikifananishwa na safu ya klabu moja ya Uingereza, Liverpool. Hii inatokana na kuwa na idadi ya magoli yaliyo katika uwiano mzuri unaoendana. Meddie Kagere akiwa na magoli sita, Clautos Chama akiwa amefumania nyavu mara nne na Okwi akiwa na magoli mawili. Hadi sasa wamefunga magoli 15 katika michuano hiyo ya klabu bingwa Afrika.
Kijana huyo mwenye miaka 23 anategemewa kuongeza nguvu upande huo wa ulinzi baada ya mchezaji wao tegenezi wa kikosi cha kwanza Charles Kalonji kupata majeraha siku alipocheza na Al Ahly; yanayomweka nje ya uwanja katika mechi hiyo.
Kocha mkuu wa timu hiyo Florent Ibege amethibitisha usajili huo mpya kwa kukubali kuufanya katika kipindi hiki akiamini kwamba ni njia pekee itakayowafanya kuweza kukabiliana na wapinzani wao. Mchezaji huyo amesaini kandarasi ya miaka mitatu kuichezea klabu hiyo kwa kipindi chote baada ya kufuzu majaribio.
Ikumbukwe AS Vita ni klabu kubwa ambayo hata 2018 walifanya vizuri sana katika michuano ya shirikisho na mwaka 2004 waliwahi kushika nafasi ya pili katika michiano hiyo ya klabu bingwa, kupitia hilo, wanaonekana kuwa na ushindani mkubwa na kuonesha changamoto kubwa ndani ya michuano hiyo hasa kwa timu wanazkkutana nazo.
Wanashika nafasi ya pili katika ligi yao ya ndani; kutokana na uzuri wa vikosi vyote viwili tutegemee kuona soka safi kutokana na aina za wachezaji kila klabu ilio nao kitu kikubwa zaidi ni ubunifu mkubwa utakaokuwepo ndani ya mechi hiyo.


Povel
Don’t miss kila la kheri mnyama