Hawajabahatika Kutwaa Ligi ya Mabingwa

Kombe la klabu bingwa ni miongoni mwa makombe yenye heshima na hadhi ya juu sana duniani. Klabu inaposhinda kombe la aina hii hupata heshima kubwa sana ndani ya msimu huo husika. Pale inapotokea klabu fulani inakosa taji hilo basi huonekana ya kwaida sana. Kila klabu hufanya kila linalowezekana angalau ipate mafasi ya kuipeleka timu yake katika michuano hiyo mikubwa. Lakini, kuna baadhi ya wachezaji wamedumu kwa kipindi kirefu katika klabu zao lakini hawajabahatika kabisa kushinda kombe hilo.

Sergio Aguero

Tuseme kama hana bahati tu ya kushinda kikombe hicho, alianza kuwika akiwa pale Atletico madrid ambapo baadae aliweza kuhama klabuni hapo bila kufanikiwa kukipata kikombe hicho. Pia hata baada ya kutua Man City malengo yake hayakuweza kufikiwa kitu ambacho bado hajakipata katika maisha yake ya soka. Ni mchezaji anayependwa sana na mashabiki kutokana na umahiri wake anapokuwa uwanjani. Ahadi yake aliyoiweka katika soka ni kwamba hatoweza kutundika viatu vyake bila kuwa na taji hilo. Umri nao unamruhusu tumpe muda.

Gabriel Batistuta

Mashabiki wa soka walimpa jina la ‘Batigoal’ kutokana ma uwezo wake. Alijiunga na Roma miaka ya 2001 akitokea Fiorentina. Ambapo aliweza kustaafu na klabu hiyo mwaka 2005. Pamoja na hayo hakuwahi hata mara moja kunyanyua au kupata medali inayotokana na kombe hilo lenye hadhi kubwa duniani. Alifanikiwa kushinda vikombe vingi katika ligi zote alizopitia lakini hakubahatika kunyanyua kombe hilo maishani.

Robert Lewandowski

Ni mshambuliaji hatari sana kuwahi kuwepo katika soka, lakini hajabahatika bado hadi sasa kuchukua taji hilo. Ana bahati ya kuingia mpaka hatua za juu kabisa lakini huishia kutolewa tu na kuachia kombe hilo kwa wapinzani. Msimu wa 2012/13 akiwa na Borussia, alifanikiwa kupanda hadi hatua ya nusu fainali lakini hakuambulia kitu. Hata alipojiunga na Bayern ambayo anaichezea hadi sasa hajawa na bahati ya kunyanyua kombe hilo.

Micheal Owen

Pamoja na historia kubwa aliyoijenga katika soka hakuwahi kufanikiwa kunyanyua ndoo ile. Ushindi wake wa Ballon d’Or haukuweza kumsaidia kupata tuzo hiyo pamoja na kuwa na bahati ya kuzunguka katika klabu nyingi kubwa kama Man United, Real Madrid lakini kombe hilo kwake ilikuwa ni kama picha tu, hadi anastaafu hakubahatika kabisa.

Wapo wachezaji wakubwa wengi sana ambao kombe hilo wameishia kulitazama tu bila kulipata. Wengine bado wanashiriki ligi mbalimbali na wengine walkkwisha staafu kucheza soka.

3 Komentara

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Poleni sana.

    Jibu

    Asante kwa update za michezo

    Jibu

Acha ujumbe