Wanasaini Tu, ni Zamu ya De Gea!

Toka Manchester United ilipopata meneja mpya wa mpito bwana Ole Gunnar, wachezaji wamekuwa na ujasiri wa kuongeza mda wao klabuni hapo! Wachezaji ambao walikuwa wanasua sua kusaini mikataba mipya sasa wanafikiria kubaki klabuni hapo, na sasa ni Zamu ya golikipa wa United sasa David De Gea.

Taarifa zinaripoti kuwa nyota huyu sasa anakaribia kusaini mkataba mpya baada ya kufanya mazungumzo kwa mda fulani na klabu hiyo. De Gea alikuwa ni mmoja wa wachezaji ambao walikuwa wanasua sua kusaini mkataba mpya na klabu ikalazimika kutumia sharti la kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi iliyokuwepo kwenye makubaliano ya awali.

Wanasaini Tu, ni Zamu ya De Gea!
De Gea atakuwa analipwa pesa nyingi zaidi kama golikipa baada ya kusaini mkataba mpya.

Baada ya kuongezewa mkataba wake kwa mwaka mmoja zaidi nyota huyu wa miaka 28 mkataba wake umebakiza miezi 18. United walitarajia nyota huyu angekubali kusaini mkataba mpya mapema kiangazi kiangazi kilichopita lakini mwanzo mbaya wa kampeni ya Mourinho msimu huu ukashuhbudia Wachezaji wengi wakionyesha kuhitaji kusepa klabuni hapo akiwemo mlinda mlango huyu.

Mazungumzo kati ya klabu na muwakilishi wa nyota huyu yaliyoendelea mwezi uliopita yanaripotiwa kuwa na matunda mema huku nyota huyu akitarajia kusaini mkataba mpya. Japokuwa nyota huyu hajaweka pesa kama kipaumbele kwenye mkataba wake, nyota huyu anatarajia ongezeko kutoka kwenye mshahara wake anaolipwa wa paundi 210,000 kwa wiki hadi kufikia paundi 375,000 kwa wiki.

Mkataba huu mpya ambao mlinda mlango huyu anatarajia kusaini utamfanya kuwa kama golikipa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.

Kufika kwa Ole Gunnar Solskjaer pale Old Trafford kumeshuhudia wachezaji wakibadilika kabisa wakiwa na morali tofauti na ile waliyokuwa nayo kipindi cha mwisho cha meneja Jose Mourinho. Bila shaka wachezaji walikuwa na msuguano na meneja huyu aliyesepa klabuni hapo siku za mwisho za majukumu yake pale Old Trafford.

Nyota ambao wameshasaini mikataba mipya ni pamoja na  Anthony Martial , Phil Jones, na Scott McTominay. Ander Herrera na Ashley Young  nao wanatarajiwa kusaini mikataba yao hivi karibuni.

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Ni noma sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.