Sarri Hatamzuia Hazard Kusepa!

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarru amesema kuwa hatamzuia nyota wa klabu hiyo Eden Hazatd kusepa klabuni hapo kufuatia mpango wake wa kujiunga na Real Madrid.

Nyota huyu amekuwa akizungumiwa kuhusu kuhama kwake klabuni hapo kwa karibu msimu mzima huku ripoti za hivi karibuni zaidi zikiripoti kuwa nyota huyu tayari alikuwa ameshafanya maamuzi kuhusu hatma yake klabuni hapo na soka lake kwa ujumla.

Meneja Sarri ameamua kusisitiza kuwa yeye hayupo kwa ajili ya kuwa kikwazo cha nyota huyu kuondoka klabuni hapo, japokuwa atakuwa na furaha nyota huyu anayemtaja kama mchezaji bora duniani kubakia Chelsea, pia anapenda zaidi kumuona nyota huyu akiwa na furaha.

Sarri Hatamzuia Hazard Kusepa!
Hazard alikuwa na ndoto ya kuchezea Real Madrd toka alipokuwa mtoto.

Kwa sasa suala la Hazard kusepa mwisho wa msimu huu limebaki mikononi mwake kuamua kama ataenda kuungana na klabu ambayo amekuwa akiipenda toka alipokuwa mtoto au kumaliza soka lake na Cheslea.

Kwa mujibu wa Sarri, yeye huongea mara nyingi lakini huwa ni kuhusu nafasi yake uwanjani sio kuhusu tetesi. Kwa upande wa Real Madrid wao wamekuwa na uhitaji mkubwa wa staa aina ya Hazard toke walipomuachia CR7 kwenda kule Juventus.

2 Komentara

    Pengo kuwa sana kwa Chelsea

    Jibu

    Maamuzi yake mtu kuwepo sehemu hanayo hipenda

    Jibu

Acha ujumbe