Mwezi 1 Washikilia Kibarua cha Mtu!

Matajiri wa Chelsea wanaonekana kutopendezwa na mwenendo wa klabu hiyo hadi sasa, kutokana na kupokea vichapo mara kadhaa kitu ambacho kwao sio cha kawaida kabisa. Kutokana na kelele hizo ni rahisi sana kusema kwamba hali ya sasa ndani ya kikosi hicho ni nafuu zaidi ya kikosi kingine.

Huo unaweza kuwa mtihani mkubwa sana kwao kutokana na mechi ambazo anaenda kukabiliana hapo mbeleni akiwa na Manchester United wikiendi hii katika kombe la FA, huku akirudi tena uwanjani na Man City katika kombe la ligi. Kitu hiki kinaweza kuwa mtihani mkubwa sana kwa Sarri kutokana na aina ya timu anazokabiliana huku akipigana kutetea kibarua chake kisiweze kuwa rehani.

Tujikumbushe

Inakumbukwa kwamba Sarri alichukua kikosi hicho kutoka kwa Conte ambaye alitimuliwa baada ya kushindwa kuendana na falsafa za tajiri wake kitu kilichomfanya tajiri huyo kumkatisha na kumpa nafasi ya kuchagua kule kunakomfaa na kumpa kibarua hicho Sarri ambaye naye kwa maendeleo ya klabu yake bado anasuasua kupata matokeo mazuri yenye kumjenga mtoto.

Walianza msimu vizuri sana na kufanya wengi kuamini kwamba ingekuwa vigumu kikosi hicho kuweza kupitwa nafasi ya nne na klabu iliyokuwa nafasi ya sita na kuonekana kama isingeweza kupata matumaini ya kurejea nafasi za juu kabisa kwenye ligi hiyo pendwa. Lakini kwa sasa imepoteza mwelekeo kabisa na kuwa nafasi ya sita kitu ambacho kwa upande mwingine kisingetokea katika soka; ni suala la subira.

Kwani wanakwama wapi?

Baadhi ya mapungufu ya wazi yanayoonekana ndani ya kikosi hicho ni kukosa muunganiko na hali ya kupigania kuweza kuipa timu yao matokeo. Suala la kupoteza mechi kwa idadi ile ya magoli ni jambo linaloonekana kwamba kikosi hicho kwa sasa hakina muunganiko mkubwa wenye nia ya kutafuta matokeo mazuri ambayo kwa namna moja nguvu yao ingesaidia kikosi hicho kusonga mbele zaidi.

Sarri hajawa na mwenendo mzuri kwa mechi hizi za usoni pamoja na kwamba kikosi hicho hakijafanya usajili mzito wenye kuridhisha zaidi ya Pulisic ambaye naye bado hajaungana na kikosi hicho pia Higuain ambaye anapigana kuendana na mifumo ya klabu hiyo na ugumu wa ligi ya Uingereza kwa wakati uliopo kutokana na yeye kuwa na wenyeji zaidi wa ligi nyingine ambazo ni tofauti kidogo kiushindani na ligi hiyo ya Uingereza.

Ni sahihi kulaumu?

Japo kwa aina ya kikosi alichonacho sio wakati sahihi kuweza kujipa majibu kwamba wakati wake kuendelea kusalia kikosini hapo umetosha, itakuwa sio sahihi maana hakuna mabadiliko makubwa ya kikosi yamefanyika kuweza kumpa nguvu ya kuwa na wachezaji mbadala wengi ambao angeweza kuwatumia kupata matokeo. Bado anastahili kupewa muda wa kufanya makubwa zaidi pia.

2 Komentara

    Asante kwa taarifa mzur meridianbet

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.