Baada ya PSG kufanikiwa kuwachapa Manchester United 2-0 kwenye gemu yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne, timu zote mbili sasa ziko kikaangoni wakiwa na tuhuma za kujibu kwa Uefa. Kesi zao zinafanana, mashabiki ndiyo wahusika wakuu!
Manchester United wao wanatuhumiwa kwa kurusha vitu, chupa za maji na vinywaji vingine ambavyo mashabiki waliingia navyo dimbani Old Trafford, na pia kuzuia njia za zenye ngazi.
PSG wao pia wamepatikana kwenye tuhuma za kurusha vitu uwanjani na kufyatua baruti za moto, uharibifu pamoja na usumbufu.
Mamlaka inayoshughulikia mambo ya nidhamu ya Uefa inatarajia kusikiliza tuhuma za klabu hizi zote tarehe 28 Februari.
Ingekuwa bongo, ni kama Yanga na Simba vile na kesi za kuvunja viti pale taifa! Inadaiwa kuwa viti zaidi ya 800 vilivunjwa upande wa wageni dimbani hapo pamoja na uharibifu mwingine.
Taarifa zinabainisha kuwa kuna uharibifu kiasi ukihusisha pia baadhi ya vyombo vya usajili na kitu kinachokwamisha usafirishaji wa baadhi ya mashabiki katika gemu.


Furahav
Psg iko vizuri.