Pamoja na kuwa na ligi nyingi sana duniani lakini kuna ligi chache zinazopewa sana heshima na kufahamika na watu wengi, na wakati mwingine hata umaarufu na kufuatiliwa kwa ligi hizo kupo juu sana. Afrika ni miongoni mwa bara linalojitahidi kuuenzi mchezo huo wenye hadhi kubwa sana duniani; kwa kuwa na timu nyingi zinazocheza ligi mbalimbali zinazofahamika sana ndani na nje ya bara la Afrika. Zifuatazo ni ligi tajiri zinazopatikana ndani ya bara.
Ligi kuu ya Misri
Haina ubishi wa namna yoyote hiyo ndiyo ligi tajiri sana barani Afrika kwa sasa ikiwa na utajiri wa yapata £143.87M. Ligi hiyo imeendelea kutawala michuano mbalimbali mikubwa ikiwemo ile ya CAF Champions League na ile ya Kombe la Shirikisho. Kuna klabu kubwa sana na maarufu kama Al Ahly, Zamalek, Ismaily na nyingine nyingi na ligi yao ina jumla ya timu 18 zinazoshiriki.
Ligi kuu ya Morocco [Botola Pro]
Ni miongoni mwa ligi ambazo zina ushawishi mkubwa sana barani Afrika kutokana na aina ya wachezaji ambao wana sifa kubwa sana katika baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya. Wapo wachezaji kama Mehdi Benatia na Achraf Hakimi ambao wanakipiga katika klabu zenye majina makubwa sana. Pia, ligi yao ina jumla ya klabu 16 zinazoshiriki huku wakiwa na jumla ya wachezaji 461. Kuna klabu kubwa kama Raja, WAC Casablanca na FUS Rabat; huku wakiwa na utajiri mkubwa unaokadiriwa kama £134.28M.
Ligi ya Afrika Kusini [ABSA Premiership]
Bila shaka hii ndiyo ligi maarufu sana duniani na Afrika kwa ujumla kutokana na kurushwa mara kwa mara mbele ya vyombo vya habari ikiwemo DSTV. Na hii ndiyo huonekana ligi bora Afrika kutokana na umaarufu wake na matumizi ya viwanja ambavyo kwa asilimia kubwa viliachwa baada ya fainali za kombe la dunia 2010. Japo sio hivyo tu masuala ya kisiasa nayo yakapelekea kukua sana. Na utajiri wake unakadiriwa kufika £130.91M.
Ligi ya Algeria [Ligue Professionnelle 1]
Inahusisha klabu 16 na wachezaji 436. Pia, ubora wa ligi hii umepelekea uwepo wa wachezaji kama Riyad Mahrez na Yacine Brahimi, na wanafikiriwa kuchangia timu zetu kiwango fulani kinachojadiliwa ndani ya taifa hilo.
Ligi ya Tunisia [Ligue I Pro]
Taifa hili lina klabu kubwa na yenye heshima kubwa sana inayofanya kazi vizuri na yenye kujiamini kama kweli kile wanachokifundisha hapo ndicho kinachoendana na matendo yake. Baadhi ya klabu zinazofanya vizuri ni Esperance de Tunis. Na utajiri wake ni £81.32M; wenye klabu 14.


Furahav
Kumbe wafrika nao wamo ila hawavumi.
Issa
Afrika pesa ipo