Soka sio kushuhudia magoli tu namna yanavyofungwa nyavuni bali inachangiwa na ule ufundi unaooneshwa na wachezaji uwanjani ili kuyapata magoli hayo, na hapo ndipo tunasema mchezaji fulani amekamilika na anafaa kuitumikia klabu fulani kubwa. Watu kama Lionel Messi, Ronaldinho, Diego Maradona, Johan Cruyff, Pele, George Best, Garrincha, Ronaldo Luís Nazário de Lima, Okocha na Zidane ni watu ambao ni hatari mno katika sekta hii.
Neymar Jr
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona anatisha sana akiwa na mpira na ni jitihada kubwa sana inahitajika kuweza kumkaba ili uweze kuumiliki mpira kutoka kwake; wachezaji wengi wamekuwa wakijaribu tu kumchezea mpira wa nguvu ili waweze kumkaba kutokana na maudhi aliyonayo akiwa na mpira uwanjani.
Hatem Ben Arfa
Rennes wamekuwa na ingizo hilo katika nafasi hiyo kwa kuonekana kuipa uhai timu hiyo katika msimu huu. Ameifungia timu hiyo magoli manne na kuchangia upatikanaji wa magoli mawili katika mechi alizozicheza msimu huu. Amekuwa hatari sana akiwa uwanjani kwa nafasi ya kuuchezea mpira.
Adnan Januzaj
Mchezaji huyo aliyewahi kuhudumu United ameingia kwenye rekodi hiyo kwa kuwa mchezaji msumbufu sana anayeweza kuuchezea mpira kwa namna ya pekee sana akwa uwanjani. Japo hajawa na msimu mzuri ila amepata kufanya vizuri katika mechi kadhaa anazozicheza.
Lionel Messi
Amekuwa kwenye ubora wake msimu huu kwa kuweza kufunga magoli 21 hadi sasa ndani ya ligi hiyo. Anakaa katika historia nyingine ya kuwa mchezaji maridadi wa kabumbu akiwa uwanjani kwa kuwafanya wapinzani kumuogopa wakati mwingine kutokana na uwezo wake.
Youcef Atal
Raia huyo wa Nigeria amekuwa hatari katika ukuta wa Nice kwa kufanya makubwa sana uwanjani. Uwezo wake wa kuuchezea mpira unawafanya makubwa wengi barani Ulaya kuanza kumvizia kuhitaji huduma yake.
Hazard
Sio rahisi kucheza na Hazard na kujaribu kuuchukua mpira kwake kama hujajipanga. Ni mchezaji wa pekee katika ligi ya Uingereza kutokana na uwezo wake wa kuuchezea mpira na kuwapa majukumu mazito walinzi wa timu pinzani kumzuia.


Mariam mtandama
Meridianbet muko vizur
Issa
Ni wachezaji hatari uwanjani