Meneja wa Barcelona Elrnesto Valverde ameangusha saini kwenye mkataba mpya unaomuongezea mwaka mmoja wa kuwepo klabuni hapo.
Mkataba huu mpya unaendelea kumuweka klabuni hapo hadi mwaka 2020, mkataba huu pia una chaguo la timu kuongeza mwaka mmoja hivyo anaweza kujikuta anasalia Camp Nou hadi mwaka 2021.
Meneja huyu mwenye miaka 55 ambaye pia amewahi kuwa mchezaji wa klabu hiyo, alimbadili meneja wa zamani Luis Enrique Mei 2017 na alishinda La Liga na Copa del Rey kwenye msimu wake wa kwanza klabuni hapo.
Msimu huu Barcelona wamekaa kileleni kwenye msimamo wa ligi wakiwa wana pointi 51, wakiwazidi pointi 6 wapizani wao Real Madrid.
Mkataba wa Valverde ilikuwa ufike tamati mapema mwisho wa msimu huu akiwa ameiongoza klabu hiyo kupata ushindi mara 65 kwenye gemu 96 akiwa ametoa sare gemu 22 na kupoteza gemu 9 kwa kipindi chote alichokuwa meneja.


Furahav
Safi.