Kiungo wa PSG Adrien Rabiot ameamua kufanya maamuzi magumu klabu gani ataenda wakati akiripotiwa anawavutia klabu za Arsenal, Liverpool, Tottenham na Barcelona.
Nyota huyu ambaye anazivutia klabu kubwa zaidi Ulaya na duniani anadaiwa kuwa mkataba wake unafika tamati mwisho wa msimu huu pale Pac des Princes.
Ripoti zinadai kuwa nyota huyu amepanga kujiunga na Barcelona, huku akiripotiwa tayari ameshafanya makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu hiyo.
Inaaminika mshahara wake atakapoingia Barcelona utakuwa kwenye kadirio la paundi 170,000 kwa wiki wakati akitia mfukoni paundi milioni 9 kwa ajili ya ada ya mkataba huo.
Barcelona ambao walithibitisha kuwa wanamuhitaji nyota huyu mwezi Disemba, walikanusha uwepo wa makubaliano ya awali na kudai kuwa mawasiliano ambayo yalijaribiwa kufanyika yalikuwa ni moja kwa moja baina ya timu hizo.
Nyota huyu anatarajia kwenda kupambania namba na wachezaji wengine wa klabu hii kama Sergio Busquests, Arthur, Kevin-Prince Boateng, Artuno Vidal na Frank de Jong kwenye safu ya ushambuliaji ya Valverde.


Povel
Habar njema