Rudiger Amkingia Kifua Sarri

Mlinzi wa klabu ya Chelsea, Rudiger ameamua kutoa yake ya moyoni kuhusiana na taarifa zinazoendelea miongoni mwa mashabiki wa kikosi hicho kuhusu mwalimu wao na mfumo unaotumika kikosini hapo hadi kuifanya timu hiyo kukosa matokeo yanayoeleweka. Mchezaji huyo amejaribu kuangalia suala linaloendelea klabuni hapo na kusema kwamba halihusiani kabisa na maamuzi au uongozi wa Sarri.

Ameyasema hayo kutokana na hali inayoendelea kutafuna furaha ya kikosi hicho kwa kuona kwamba ni jambo gumu kwa mchezaji yeyote kuyapokea matokeo hayo lakini anachoamini yeye ni suala la utayari kwa mchezaji mmoja mmoja hadi ngazi ya klabu kuweza kujituma ili kuhakikisha kikosi kinapata matokeo yake na kurejea kwenye ushindani.

Hadi sasa kikosi hicho cha Darajani kimefanikiwa kushinda mechi zake mbili tu kati ya tano walizocheza. Na ndani ya mechi hizo wamepokea dozi za magoli mengi kitu ambacho katika hali ya kawaida kimeshusha hadhi ya klabu iliyokuwepo miaka ya nyuma kwa kuonesha ushindani ambao sio wake wa miaka ya nyuma.

Baadhi ya vipigo vizito walivyopitia Chelsea ni dhidi ya Bournemouth aliyemfunga 4-0, Manchester City 6-0 na United akashindilia zake 2-0. Mlolongo wake wa matokeo haujawa wa kuridhisha sana. Suala hili linaweza kurekebishika kabisa ndani ya kikosi hicho kwa sasa kama Rudiger anayoliona jambo hilo kwa sababu kuna wakati kikosi hicho kilikuwa na matokeo mazuri chini ya kocha huyo lakini kadri siku zinavyozidi kwenda matokeo yakabadilika ghafla.

Kikubwa ni kunwamini Sarri kwa kuendelea kumpa muda na kujaribu kubadili aina yake ya mfumo ambao unaonekana kuwatesa baadhi ya wachezaji kutokana na majukumu waliyopewa ndani ya mfumo mpya. Kwa kufanya hivyo itakuwa inewasaidia kutatua tatizo hilo na kuruhusu wachezaji kufanya majukumu yao ya siku zote yaliyokuwa yanawapa matokeo chanya.

Wachezaji hao wanaendelea kuzungumza kwamba kuna wakati kweli ni vigumu kurudisha kikosi kama kilivyokuwa miaka ya nyuma; kilichokuwa na wachezaji kama John Terry au Frank Lampard lakini wanachojitahidi kufanya ni kuziishi na kuzifuata zile nyayo zao ili kuweza kuleta kile ambacho kitawafurahisha mashabiki.

Rudiger alipoulizwa juu ya ubora au ubovu wa kocha wao akashindwa kutolea ufafanuzi kuhusu suala hilo kwa kusema kwamba yeye ni mchezaji na ni ngumu kuchambua akiwa kama mchezaji kwamba anawafaa au hawafai kwa wakati uliopo; kwake yeye anaona kuna haja ya kuuchungulia kwa jicho la pekee mfumo wa uchezeshaji kabla ya kufanya lolote kwa sasa. Na kuona kwamba wanachokiangalia kwa sasa ni mechi yao ngumu ya EFL dhidi ya Manchester City.

4 Komentara

    Uko sahii

    Jibu

    Vizur

    Jibu

    Sarri mbinu zake za kizaman hapa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.