Staa wa Paris Saint German -PSG Neymar ametoboa siri kuwa alimwaga machozi kwa siku 2 mfululizo baada ya kupata jeraha lake la pili mwezi uliopita lililofanana na lile alilolipata mwanzo na kutumia miezi kadhaa kuwa vizuri na kurejea dimbani.
Kwa sasa nyota huyu anaendelea vyema akiuguza jeraha lake, amelazimika kuwa nje ya dimba kwa mda wea wiki 7 baada ya jereha. Neymar alipata jeraha kama hili la sasa msimu uliopita mwezi Februari na kukosa kipindi kilichobakia kumaliza msimu.
Hiki kimekuwa kikwazo kwa nyota huyu ambaye analazimika kuwatazama wanatimu wenzake kwenye TV kwa sasa.
Neymar anasema “nililia kwa siku mbili nikiwa nyumbani. Imekuwa ngumu zaidi. Mara ya kwanza nilipojiumiza nilijisemea kuwa inatakiwa nifanye upasuaji, hii kitu lazima iwekwe sawa haraka iwezekanavyo. sikuhuzunika sana. Lakini wakati huu, nilikuwa na wakati mgumukukabiliana na hili”

