Vijana wa Paris Saint Germain -PSG, Angel Di Maria na Kylian Mbappe wanamkosha meneja wa klabu hiyo bwana Thomas Tuchel kwa ushirikiano wao kama pea wanavyokuwa dimbani.
Watabe hawa wa Liguue 1 wamefanikiwa kundeleza ubabe wao licha ya kuwepo nje kwa pea ya Edinson Cavani na Neymar.
Klabu hii wamefanikiwa kushinda gemu 5 mfululizo kwa michuano yote huku wakiwa na gemu nyingine leo dhidi ya Nimes.
Jinsi wawili hawa. Di maria na Mbappe wanavyofanya kazi imekuwa ni pea bomba sana inayomfurahisha Tuchel.
“Di Maria anacheza kama mshambuliaji wa pili akiwa na Kylian (Mbappe), ambayo ni nzuri sana kwa sababu anao ubora faa pembeni ya kylian kuwa mfungaji. napenda sana hii. Hawa ni wachezaji bora zaidi kupata magoli.” -Thomas Tuchel
Kwenye gemu 5 walizocheza, wamepata jumla ya magoli 12 na kufungwa goli moja. Bila shaka Tuchel atapendelea zaidi kuitumia pea hii ya Mbappe na Di Maria.

